Mambo Matano ya Kufahamu Baada ya Kadi za UDART Kuanza Kutumika

Abiria wa mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es salaam leo June 20 2016 wameanza kutumia kadi maalumu za kielektroniki badala ya tiketi. Mfumo huu ambao utamuwezesha abiria kuweka fedha katika kadi hio kwa kutumia mitandao ya simu na utasaidia kupunguza msongamao katika vituo vya ukataji tiketi.

HAYA NI MAMBO MATANO YA KUFAHAMU

1.Unapokwenda kununua kadi utapewa maelekezo ya namna ya kujisajili, kuna namba ya *152*22# ukipiga namba itakupa maelekezo, utachagua kwenye menu litatokea neno DART itakupa maelekezo kama unajisajili utatakiwa kujaza namba ya kadi, utajaza majina yako na utaweka namba yako ya siri.

2.Ukipoteza kadi hatua ya kwanza unaweza kuifunga isitumike na mtu mwingine kwa kubonyeza *152*22# unachagua DART itakuja option ya kuifunga.

3.Kadi ikinunuliwa tayari ina muda wa kusafiri, kwamba hutalazimika kufanya Top up  baada ya kuinunua, kadi utainunua 500 lakini utakuwa na muda wa kusafiri wa sh 4500, baada ya kuwa umeshainunua unaweza kusafiri muda huohuo.

4.Ukipoteza kadi na ukitaka kupata mpya, kama iliyopotea ina muda wako wa kusafiri taarifa zako zitasaidia kupata kadi mpya na utarudisha pia salio lako ambalo litakuwa limebaki.

5.Wanafunzi wataendelea kutumia tiketi kwa sababu mfumo wa tiketi pia bado utatumika sanjari na matumizi ya kadi, usajili wa mwanafunzi ili wapate kadi zao utachukua muda.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Itachukua muda mpaka wabongo waelewe nini maana ya kadi. kazi ipo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad