Mambo Matano Yaliyoibuka Wakati wa Mahojiano ya Zitto Kabwe na Polisi

Leo June 08 2016 Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefika Makao makuu kanda maalum ya Dar es salaam, ikiwa ameitikia wito wa polisi. Zitto amefika kituoni hapo na ametakiwa atoe maelezo kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa June 5 2016.

Kupitia ukurasa wake wa facebook chama cha ACT Wazalendo kimeainisha masuala matano muhimu yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.

1.Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa ‘Kujenga Chama’ Lakini Chama Kilizindua “Operesheni Linda Demokrasia”.

2. Kusema “Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini” 

3. Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni “Vilaza” 

4. Kumgombanisha Rais na Wananchi kwa Kusema “Yeye anajifanya Rais wa Masikini (Huku akiwakashifu hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita “Vilaza”) na hivyo kumgombanisha na wasio Masikini” 

5. Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla 

Kupitia ukurasa huo wametoa taarifa kuwa maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa yote hayo yanaangukia kwenye Kifungu Cha 89(1)(a) cha Penal Code, Yaani “Kutumia Maneno ya Matusi yenye Kuweza Kuvunja Amani” (Abusive Language).

Jeshi la Polisi limemuomba Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi. Mwanasheria wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani Juu ya Suala Husika, Na Kwamba Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli Na Undani wa Masuala hayo Mahakamani.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hiyo Dogo bado Tu ... Nasoma hapo mwanasheria je unanua kuwa Kuna High treason charges..zitto wewe Ni mtovu WA nidhamu Na mchochezi.. Na umeweza kutumia uongo Na kuchukua kibali Na kutumia kwa lengo lisilokiwa kusudiwa.. Sasa jua Hilo Ni kosa..madaa Na maudhui Ni chochezi...Unaelekea kubaya jirudi kabla hujafika haya.. Na tcra wana hali ya kusitisha hiyo fesibuku nanake Ina lengo la kuchafua utulivu...Kua KIAKILI mwansiasa Uchwara uliyeshindwa siasa

    ReplyDelete
  2. Wewe mshamba Zitto nakushauri upumzike huu ni mwezi mtukufu acha watu wasali na kufanya vitu vya maendeleo. Kama huna sera basi achana na siasa. Wasted of time....Tumekuchoka fyuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Makubwa haya
    Tuliwacheka majirani
    Na kwetu yanakuja

    ReplyDelete
  4. Magu jaribu kumuiga jk sio kila kitu polisi.mbona jk ametukanwa sana ila kafanya hasikii yamepita kabaki Hana lawama na mtu zaidi ya lowasa. Laana ya luwasa ndio inamaliza taratibu. Jamani malipo duniani mbinguni batazzz

    ReplyDelete
  5. ikibidi apewe adhabu akiongea utumbo anaona sifa tumemchagsua wenyewe ccm ndio ilio kukuza wewe vp uropike uvyo hivo zito kweli ulienda shule? siasa haitaki wenye tabia kama zako kuwa akili

    ReplyDelete
  6. Zitto Kabwe Zitto! Siasa siasa siasa...Unawaona watu kama kina mlema / Slaa / na karibuni mbowe na wengine ambao walikuwa na Jina... sembuse wewe mtoto wa kijiweni unataka uwe kila siku midomoni kwa watu sasa hebu niambie wewe na wema nani zaidi.. febuku au instaglamu ipi bola? Tafuta majukumu ya familia... Manake ikiwa huna hutojua au kufikiria sahihi unako kwenda.. na ulipataje ubunge?? Ulinunua au ulihonga au ulizawadiwa bila ya wewe kutaka inaonesha na kudhihiri kuwa huna lolote wala chochote....na kibaya zaidi huu ubunifu wako mpya ni mbaya na utakupeleka pabaya.... Je unalielewa hilo????????

    ReplyDelete
  7. Huyo Dogo inabidi tumwangalie maana ana dalili za kuwa si Mtu wa hapa kwetu... Uzalendo hana na tabia hizi ni zanchi jirani... Naomba wahusika idara ya Uhamiaji waaliangalie hili swala...asije kuwa ni mtu wa Nyakabiga au Bwiza!!

    ReplyDelete
  8. Jamma amesha poteza netiwoki inarudi na kugonga mstimu.. au betri ndiyo imebaki kibaa kimoja!! mawasiliano yanakuwa matatizo kwenye nywele.

    ReplyDelete
  9. Zito hajitambui,angalia hata watu tuliokuwa kwenye mkutano wako siku ile,hatukuwa kama tulivyozoeana,kwanza tulikuwa wachache,hakukuwa naushirikiano wa sana,ulichokielezea hakikutegemewa na wengi,na zaidi tunakuona kama ndumila kuwili,kuna wakati unaonekana kama uko chadema.Pumzika kwanza,jenga familia yako,pengine baadae utapata ushauri mzuri.

    ReplyDelete
  10. Kumsaidia Kijana ni bora tuchange ili tumpatie Jiko.. Ukuta nne kila siku zinachanganya mpaka unachanganyikiwa... Wasamaria wema.. MPO??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad