Manispaa ya Ilala imekusanya Sh1 bilioni ndani ya siku tano, ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanafikia lengo la kupata mapato ya Sh55 bilioni katika miezi sita ya mwanzo ya Serikali ya awamu ya tano.
Meya wa Ilala, Charles Kuyeko aliyembatana na Naibu Meya Omary Kumbilamoto na Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Isaya Mngurumi amewaambia wanahabari leo kuwa mapato hayo yamekusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwamo kodi ya majengo.
Kuyeko amesema mafanikio hayo ya kukusanya kiasi hicho cha fedha pia, yametokana na kikosi kazi kilichoundwa na manispaa hiyo ambacho kina lengo ya kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa muda wa mwezi mmoja.
“Kila hatua tutakayofikia tutakuwa tukitoa taarifa. Kuhusu kampeni hii ya ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato,” amesema Kuyeko.
Manispaa ya Ilala Yakusanya Sh Bilioni Moja Ndani ya Siku Tano
1
June 13, 2016
Tags
Hapa ni kazi tu
ReplyDelete