Manji Aendelea Kusubiri Majibu ya Barua Yake Aliyomwandikia Rais Magufuli Kuhusu Sakata la Coco Beach


Mwenyekiti wa Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Yusuf Manji amesema bado anasubiria majibu kutoka kwa Rais John Magufuli juu ya sakata la kuendeleza ufukwe wa Coco, maarufu Coco Beach uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kumwandikia barua Desemba mwaka jana.

Manji alisema anatamani suala hilo limalizike kabla ya kuondoka rasmi katika kampuni hiyo mwezi ujao, na kwamba tayari alishamwandikia barua kiongozi huyo wa nchi juu ya usahihi wa mchakato wa zabuni wa kuendeleza eneo hilo la ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Mfanyabiashara huyo anasema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa Serikali kurudiarudia suala hilo na kusababisha kuwa maarufu kuliko hata Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, suala la Coco Beach ilikuwa ni sehemu ya biashara na kwamba zabuni hiyo walishinda baada ya kutimiza masharti yaliyokuwa yamependekezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, lakini cha kushangaza hali imekuwa tofauti.

Mfanyabiashara huyo alifikia hatua hiyo kufuatia Rais John Magufuli kutangaza eneo hilo liendelee kutumika na watu wa kawaida kwa kile alichosema kuwa kuna mfanyabiashara ambaye anatumia fedha kuwahonga baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo ili kumiliki eneo hilo.

Rais Magufuli ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa wafanyabiashara alisema; “Inanifadhaisha sana kuona mfanyabiashara tajiri akihonga maofisa kutumia vibaya fedha za umma kwa manufaa yake binafsi na wakazi kutoka mazingira duni wakishindwa kutumia ufukwe huo kuogelea na kuburudika.”

Hata hivyo, Manji alisema kuwa kampuni yake ilikuwa ikilihitaji eneo hilo kuliendeleza kwa ajili ya biashara na kuhudumia wananchi hivyo iwapo Rais ataridhia linyang’anywe licha ya kushinda zabuni na mahakamani, hawatakuwa na hatua nyingine ya kufanya.

Alisema Rais aliyasema yake na Mahakama ilishafanikisha ushindi wa awamu ya kwanza na Serikali baadaye ilikata rufaa na kwamba mtu yoyote akitaka kusoma kwa nini walishinda kesi ya awali, hukumu iliyotolewa inajieleza.

Manji alieleza kuwa ingekuwa eneo lile linahitajika kwa matumizi binafsi hata wangemwambia aliachie na achukue Jangwani angekubali, lakini kampuni isingekubali kwa sababu eneo lile lilitafutwa kwa ajili ya biashara na mbadala wowote huenda usiwavutie wanahisa.

 “Coco Beach siyo nyumbani kwangu na wala siyo sehemu ambayo lazima niwe nayo au nisiwe nayo. Ni sehemu ambayo kampuni ilihitaji kwa ajili ya uwekezaji,” alisema Manji.

“Wanahisa walitaka kuwekeza lakini iwapo halitapatikana, hawajatufungia milango ya kiuwekezaji kwa kuwa Coco Beach siyo sehemu moja tu duniani ya kuwekeza.”

Tayari QGL ilishaingia ubia na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mwishoni mwa mwaka jana kutekeleza mradi wa Dola 250 milioni za Marekani (Sh537.5 bilioni) kuendeleza eneo la Bwawani, kwa kuikarabati hoteli hiyo na kujenga mji wa kisasa ambao utakuwa na huduma zote za kisasa katika visiwa hivyo.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndio hawa mafisadi wakubwa wala rushwa wa nchi hii wanawatumia wanasiasa uchwara aina ya Zitto Kabwe waje na visingizio vyao vya Demokrasia ili waendelee kuitafuna Nchi hii. Huo ni ujanja wa mafisadi tumeishaugundua na hao wanasiasa wasiojielewa aina ya akina Zitto na Dj Mbowe ndio imekula kwao. Hiyo Coco Beach hataipata na ni kwa sababu ni mali halali ya Watanzania wote na sio mali ya mtu binafsi.

    ReplyDelete
  2. Coco beach magufuli usitoe ng'o
    Yetu maskini
    Wapewe jiji
    Kama manji anapesa bongo kuna beach tele hazina hata watu ajenge na hoteli matajiri wenzake
    Yanga hamtoshi

    ReplyDelete
  3. Manji... Uliipata Hii wakati wa Hewa Kujaa kila Mahali.. Itakuwa ni Busara na Uzalendo ikiwa wewe mwenyewe Utaitoa Msaada au Sadaka katika Halmashauri uliyo ichukulia ,,, Hapo itakuwa umefanya lamaana... Na ni Busara kuona wananchi na nchi wanalitumia hilo eneo..Kama unenielewa utakuwa umeelewa

    ReplyDelete
  4. Msioelewa tembeeni duniani angalieni sasa coco imeoza inanuka serikali inakusanya hela za parking tu 😅😅😅😅 ile sehemu ya baishara lazima itengenezwe ipendeze ingieni hapa muone www.scheiveningen.nl

    ReplyDelete
  5. Polen Sana Manji. Kwa awamu hii utasoma namba wewe na hao wenzako mliyefanya nchi kama shamba la bibi kipofu. Hapa kazi tu...

    ReplyDelete
  6. Hapo Zitto katoka wapi? au Yanga inatoka wapi. Kwa nini usisema habari za hela ya familia kama ambavyo huwa anasema kuliko kuwataja watu wasiohusika, zito wala mbowe hawapo kwenye jiji la kinondoni waliopitisha zabuni hii. pole siasa yako itakufikisha vibaya

    ReplyDelete
  7. mashabiki ya simba a.k. a MACHURA ndiyo yanaleta mambo ya Yanga kwenye issue isiyohusu michezo!! coco beach siyo kwamba Manji anataka miliki, yeye anataka akodishwe ili apaendeleze pawe sehemu ya kuvutia.

    ReplyDelete
  8. Tatizo kuna vyura wasioelewa mambo ndio maana katika issue nyeti wao wanarukaruka tuu,acheni ujinga pale ni pa kuendelezwa kama si manji basi Mohamed Dewji!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad