Kwa Mwendo Huu wa Diamond..Mdogo mdogo Utasikia Kaanza Kubwia na Unga Kabisa

Somo la kujaribujaribu liende kwa Diamond. Mtindo wake wa maisha unabadilika kwa kasi mno. Labda ni kwa sababu Marekani anakwenda mara kwa mara. Kuna kipindi tulimshuhudia akiwa amebandika kipini puani. Mshtuko ukaibuka, kipini tena!

Katika wimbo, Muziki Gani ambao ameshirikishwa na Nay Wamitego, Diamond mwenyewe anawashangaa wanamuziki wa Hip Hop: “Hata mimi mengi nayajua ila wewe mtemi utaanzisha utata, mchezo wenu kutoboa pua bora ninyamaze usinipige mbata.”

Natambua kuwa kile kipini alibandika, hakutoboa pua, ila tofauti ni nini. Anayetoboa lengo lake ni kuvaa kipini kama ilivyo yeye anavyobandika. Diamond anataka kuwa kama yule tajiri, amejipamba, sasa anaamua kuvaa na vipini puani.

Dunia inakwenda kwa kasi mno! Diamond wa leo ametandaza dhahabu mdomoni. Meno yake sasa hivi utadhani ya Lil Wayne, Tatoo ndio usiseme , Shida kubwa ni kwamba hata kuongea siku hizi anapata tabu. Mdomo wa Diamond umekuwa mzito.

Akiwa anazungumza utafikiri ana mapengo ya chini kwa jinsi anavyopata wakati mgumu. Ndipo alipofikia, Umarekani unamtawala. Siku zijazo tunaweza kuona mengi zaidi yanajitokeza kwa bwa’mdogo huyo aliyetokea Tandale na kufanya matukio makubwa ya kimuziki barani Afrika.

Nachukua fursa hii kumkumbusha Diamond kutambua ustaa siyo mpaka aonekane Mmarekani. Mbona alikuwa hana kipini puani na aling’ara Afrika? Mbona hakuwa na dhahabu mdomo na alimpata mwanamke wake cheupe wa Kiganda, Zari The Boss Lady?

Athari kubwa ya kuigaiga ambayo Diamond anaenda nayo, ipo siku ataambiwa kuwa akina Lil Wayne na Chris Brown wanakuwa vichaa walivyo kwa sababu huwa wanaonja unga, naye itabidi aonje. Na akifika huko, moja kwa moja atageuka kuwa teja. Simuombei afike huko, ila kwa mwendo wake wa kuigaiga, sitashangaa siku nikisikia Diamond anavuta madude.

Na Luqman Maloto

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwambie na Wema alietimuliwa kwenye nyumba kwa wizi wa umeme. Aliejivalisha matambara akiyaita mimba. Alienyang'anywa gari na TRA. Alieweka tako la kichina. Mwambie ametutosha na michirizi yake.

    ReplyDelete
  2. Hapa mipasho naye ajibu
    Kwa waliosema eti nywele miliion 2
    Wasanii lazima wapashane eti
    Mashsbiki tupate uroda
    Kwani bungeni uroda wa live hatuuoni tena ccm Hoya

    ReplyDelete
  3. Hapa mipasho naye ajibu
    Kwa waliosema eti nywele miliion 2
    Wasanii lazima wapashane eti
    Mashsbiki tupate uroda
    Kwani bungeni uroda wa live hatuuoni tena ccm Hoya

    ReplyDelete
  4. Braza umeongea ukweli,I see your point.
    diamond, take that pieceof advise.

    ReplyDelete
  5. Diamond unachusha kinoma kwa hayo meno yako ya dhahabu. Tafadhali bandua hiyo dhahabu maana huo mdomo chini umetepeta

    ReplyDelete
  6. Diamond unachusha kinoma kwa hayo meno yako ya dhahabu. Tafadhali bandua hiyo dhahabu maana huo mdomo chini umetepeta

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad