Messi Ajiuzulu Baada ya Kukosa Penalti

Mshambulizi wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amestaafu kutoka soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.

"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Nimefanya kila niwezalo.''

''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.

Mshambulizi huyo ameisaidia mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.

Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.

Argentina imeshindwa katika fainali tatu za kimataifa.
Argentina walilazwa moja kwa nunge na Ujerumani katika kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil.

Timu hiyo aidha imeshindwa na Chile mara mbili katika fainali za mchuano wa Copa America kupitia kwa mikwaju ya penalti.

Messi vilevile alikuwa katika kikosi kilichoshindwa na Brazil katika mchuano huo wa mwaka wa 2007 wa Copa America .

Argentina walitoka sare ya 0-0 baada ya muda wa kawaida na ule wa ziada.

Hata hivyo Chile waliibuka videdea kwa mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti.
Messi alipoteza mkwaju wa kwanza.

Akiwa Uhispania Messi ametikisa wavu mara 453 kati ya mechi 531 alizoshiriki.
Aidha Messi ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa La Liga akiwa na mabao 312.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad