Msanii Diamond Atoa Msaada Wa Madawati 600 Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mhe. Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendelea ya mkoa.

Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu.
  
Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam.
  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. safi sana mondi

    ReplyDelete
  2. Mimi sio shabik wako Diamond ila kwahil umefany vizur nanim kukubali. Honger hiz ndo habar tunahitaj kusikia sio skendo ambaz hazin manufaa. Ukiendelea hiv nitakua shabik wako. Ushaur wang achan na skendo utakua unajijengea heshima.

    ReplyDelete
  3. hongera sana,huo ni mfano mzuri sana kwa jamii

    ReplyDelete
  4. Hayo ndo mambo ya msingi kukumbuka wenye shida,na sio kuhonga magari kwenye birthday

    ReplyDelete
  5. HONGERA SANA WCB. NI MFANO WA KUIGWA!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad