Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Tizeba apelekwa Kilimo na Mifugo

Rais John Pombe Magufuli leo tarehe 11 June 2016, amemteua Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Mhe. Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Wakati huo huo rais amemteua mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi, nafasi iliyokua ikishikiliwa na Mhe. Nchemba.

Wateuliwa wataapishwa siku ya Juma tatu majira ya saa 3:00 asubuhi Ikulu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Nchemba, Nuru imekuangaza, Nakutakia kila la kheri fanya kazi kwa uadilifu bila kujali Rangi, itikadi ya chama wala mapenzi ya nia na fikra za watu. Astahiliye haki mpe anayestahili msamaha apewe, anayestahili mvua mpe ukifanya hivyo utakuwa waziri mwema.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad