Naibu Spika Aendelea Kuwatesa Wapinzani Kwa Kuendelea Kuendesha Bunge Licha ya Wapinzani Kugoma Kuingia Bungeni

Kwa kawaida, Spika wa Bunge, Job Ndugai au naibu wake wanapokuwa na shughuli nyingine, huachia kiti hicho kwa wenyeviti watatu wa Bunge kuendesha vikao, lakini safari hii Dk Tulia amekuwa akiingia kila siku asubuhi na jioni.


Mei 31, mwaka huu wabunge wote wa upinzani walianza kususa vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo kwa madai ya kutokuwa na imani naye, hasa baada ya kuzuia hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi 7,802 katika chuo cha Udom.


Hoja hiyo iliwasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari lakini Dk Tulia alisema haikuwa na umuhimu kwa wakati huo, jambo lililozua tafrani baina ya kiongozi huyo na wabunge wote wa upinzani.


Kutokana na hali hiyo, wabunge hao walipitisha azimio la kususa vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo na tangu siku hiyo, kila anapoingia bungeni kuongoza kikao wamekuwa wakitoka ukumbini.


Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye kwa sasa yuko nchini India kwa matibabu, amekuwa akisaidiwa na Dk Tulia pamoja na wenyeviti watatu wa Bunge ambao ni Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge
Tangu wabunge wa upinzani waanze kususa vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, kiongozi huyo wa Bunge ameamua ‘kukomaa’ na kiti hicho, hatua inayosababisha wapinzani wasipate fursa ya kutia mguu bungeni.

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa kazi tu endelea mama na hongera kwanz hao eti ni wapinzan hatuwatak wabak makwao kwan hata kuwepo kwao bungeni hausaidii chochot kwan wanalet vurug na poroja bila kufany walio tumwa na wanainchi walio wachagua ili wawakilish. So watakion chamtem kuni 2020 wakat watatak kur ten. Nahap watakua wanaulizw kit gan walich kifany. Aibu kwao kwasabab hawajielew.

    ReplyDelete
  2. Anajitesa mwenyewe na vijisentii vya posho
    Hatugeuki jiwe ngoooo
    Aendeshe hao wanaomwita mama wakitegemea kuteuliwa kwenye kamati za bunge
    Ukawa jembe

    ReplyDelete
    Replies
    1. pumba hujielewi unachokiandika nenda shule na acha ushabiki wa kijinga, sizitaki mbichi hizi kumbe unazitaka

      Delete
    2. Pumba wewe usiyejuwa dunia wala akhera
      Kukubali kila kisemwacho
      Hata Kama hakina tija
      Futyyyyyyyyy
      Pumbavu

      Delete
  3. Katuka bunge vishindo awape hayo waliompigia kura
    Na akae si bungeni atembelee na majimbo asikie vishindo vyetu
    Fyuuuuuhhhhh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad