Hatimaye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson ametoa maamuzi kuhusu hoja ya wabunge kulipwa posho au kutolipwa wanapoingia Bungeni na baadae kutoka nje kwa shughuli zisizo za Kibunge.
Akisoma muongozo wake muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jioni hii baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, Dk. Tulia alisema kuwa wabunge wanaofanya vitendo hivyo hawatalipwa posho.
Alitoa uamuzi huo baada ya kurejea kanuni za Bunge akitumia kanuni ya tano fasili ya kwanza ya toleo la mwaka 2006 na maamuzi yaliyowahi kufanywa na Spika waliotangulia katika hali kama hiyo.
“Hivyo basi, kwakuwa jambo hili halikubaliki, na kwakuwa miongozo kadhaa imeshatolewa kuwasihi waheshimiwa Wabunge wasitoke nje ya ukumbi wa Bunge kwa shughuli zisizo rasmi.
"Naagiza kwamba wabunge wote wanaojisajili kisha kutoka ukumbini kwa kususia vikao vya Bunge, hawatastahili kulipwa Posho kwa siku zote ambao wamekuwa wakijisajili kuingia ukumbini na kisha kutoka ukumbini,” alisema Naibu Spika.
Wabunge wa Upinzani wamekuwa wakitoka nje ya Bunge muda mfupi baada ya kuingia Bungeni katika vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu Spika kwa madai kuwa hawana imani naye kwakuwa amekuwa akiongoza Bunge kwa ubabe na kuwapendelea wabunge wa CCM
Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa, Aagiza wasilipwe Posho wakisusa
16
June 09, 2016
Tags
safi sana maana walizoea kutuchezea hao wasilipwe kabisa maana wanafanya shughuli zao alfu posho waje wachukuwe bungeni uamzi sahihi kwani wanataka kula jasho la watanzania bila kufanya kazi big up tulia
ReplyDeletewell done
ReplyDeletewengine hapo wanaiga mkumbo sio kwamba hawapendi kuhudhuria bungeni ila wanashindwa kutokana na kuwajibishwa na chama chao lakini tunao huku tunaongea nao wanasema sisi tunawafuata wao tu lakini sio kwamba hatupendi kuingia maana baadhi ya wenzetu wanahela nje ya bunge hata wasipopata posho watapata sehemu nyingine lakini sisi tunategemea poshohiyo sasa ninachojiuliza kama wanaelewa hivyo kwanini wawafuate wao si waingie tu bungeni mbowe anawaharibu sana mwenzenu anamahela kibao fikirini kabla ya kutenda HAPA KAZI TU
ReplyDeleteTatizo wengi ni vilaza,kwa nini mtu asitumie akili yake mwenyewe na ukubali kutumiwa na Mbowe.
DeleteINAPENDEZA WASIPEWE POSHO
ReplyDeletevilaz utawajua tu wanaumia lakini wanashindwa kutoskana na macho ya watu poleni kama mnaangalia hilo
ReplyDeletewasipewe posho safi sana Tulia maamuzi mazuri
ReplyDeletewatapata huko huko wanakoenda kuzurula kazi na dawa
ReplyDeletehivi KAMBI YA UPINZANI mnakubali kushililiwa akili na Mbowe
ReplyDeleteWASIPEWE HAO WAMEZIDI NI UTOVU WA NIDHAMU,KAMA WANAJUA WATATOKA HUWA WANAINGIA KUFANYA NINI?FANYENI KAZI JAMANI ACHENI HUO UPUUZI!!!
ReplyDeleteyani ni kweli maamuzi sahihi kabisa, nashangaa sana wapinzani wasomi kabisa wanaongoza na mbowe wakati mbowe ni mjanja sana yeye anataka kuwaharibia wao ndo hana uchungu kabisa, watanzania amkeni mnaweza kujifanya mnamsimamo kutetea mgomo bungeni mwisho wa siku makakosa yote, mtu yoyote mwenye heshima hawezi kutoa kauli mbaya sehemu yoyote ile, ila wambunge wetu wanaona kupayuka bungeni ni sifa kumbe ni kujivunjia heshima..haipendezi hata kidogo ..maamuzi ni sahihi ya kutowapa posho ..HAPA KAZI TU
ReplyDeleteUamuzi sahihi na bora,maana asiyefanya kazi na asile.
ReplyDeleteNimekaa chini na kuwatafakari hawa Wanasiasa Uchwara.Nikianza na Maalim Seif Sharif Hamad, Aliwadanganya wenzake wakagoma kushiriki uchaguzi sasa wamepoteza kila kitu. Dunia ya Sasa sio win/Loose situation bali ni win/win situation.Pili, hawa wanaotoka Bungeni kila kukicha. Mchezo wanoucheza ni uleule wa win/lose situation. Wananchi tuliwachagua kwenda Bungeni kuwasilisha matatizo yetu sasa wameachana na jambo lililowapeleka Bungeni wameanza mchezo mchafu wa kutoka Bungeni kila kukicha.Kusema kweli wanatukosea Adabu.Karata wanayoicheza kwasasa itawaangamiza kama alivyo angamia Maalim Seif. Tanzania inapambana na Ufisadi wapinzani wanapinga sasa wanataka kitu gani? Inaanza kuniingia akilini kwamba hawa watu ni vibaraka wa Mabepari wa nje na Ndani. Issue muhimu za Ufisadi wa Sukari hawagusi kabisaaa. Wanazungumzia demokrasia, Hivi hao wote kuna mtu hapo anaijua vizuri tafsiri ya Demokrasia. Demokrasia bila Utawala wa Sheria haipo. Demokrasia ina mipaka yake.Mwisho wa hawa jamaa na Siasa za Majitaka unakaribia, tutawahukumu muda si mrefu.
ReplyDeleteMzalendo
nmecheka sana watapata posho uko uko pakuzululia..kweli wapinzani hamna kitu!
ReplyDeleteWatanzania wengi akili finyu.ndo maaa hskuna maendrlro ya kweli.lngswa estu wans mamilioni hawajui hski zso sheria zao.ni nchi maskini sababu hawajui kufikiti, sio aggressive watulivu ss babu ya ujinga, utaeanysmazishs kirshidi sabsbu ya uzito ws kufikiri n.a. dunk kielimu.
ReplyDeleteTatizo kubwa la hawa VILAZA ni madai yao ya BUNGE LIVE Pumbavu sana hawa hebu JPM itisha uchaguzi tuone kama watarudi mjengoni hawa Vilaza
ReplyDeleteBunge Live hawajui sisi Mtimbila hatuangalii TV saa 4 asubuhi tuko shamba na nchi hii ni zaidi ya 65% ni wakulima sasa hawa vilaza kwani tuliwachagua ili tuwaone LIVE???? Wakitoka nje ya mjengo wasilipwe posho,,, Vizuri sana