Nape Asema Lowassa ni Alama ya Ufisadi, ampa ushauri mgumu

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amenena tena kuhusu uamuzi wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupewa nafasi ya kugombea urais.

Nape ameeleza kuwa uamuzi huo uliwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanasiasa huyo aliyekuwa na nguvu kubwa ndani ya chama hicho alikuwa alama ya ufisadi kutokana na kukabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi.

“Lowassa alikuwa alama ya ufisadi, alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu walikuwa wanahusisha ufisadi na umasikini, walichoka na walikuwa radhi kuchagua hata jiwe lakini sio CCM,” alisema Nape.

Alisema kuwa angepata nafasi ya kumshauri Lowassa katika siasa, angemshauri ajiuzulu siasa kabla hajaondolewa kwa aibu katika medani za siasa.

Kadhalika, Nape alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na vyama vya upinzani ni kumpokea Lowassa ambaye amedai alikuwa amesababisha CCM kupakwa matope ya uchafu kutokana na kuwa na tuhuma nyingi.

Hata hivyo, Nape alimpongeza Lowassa kwa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu kwa kuwa uamuzi huo ulisaidia kuliweka Taifa katika hali ya amani baada ya uchaguzi.

Lowassa amekuwa akikanusha tuhuma zote zilizokuwa zikielekezwa kwake hususan tuhuma za kuhusika na sakata la Richmond lililosababisha ajiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Alijiunga na Chadema na kugombea nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vya siasa vinavyounda Ukawa.

Alipata kura takribani milioni 6 na kusaidia kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani akiweka historia ya ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye uchaguzi mkuu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nape mafisadi wapo ccm na ccm inawalea
    Kama lowasss ni fisadi mbona hamkumpeleka kotini Kama kina Mramba
    Kumbe bado anawatesa

    ReplyDelete
  2. Mbona nape unamwogop Sana lowassa? You have no point

    ReplyDelete
  3. Ndio nashangaa, mafisadi yamejaa fisiemu tele. Anzeni na hayo kwanza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anajuwa ufisadi wa kikwete na Kinana

      Delete
  4. Lowassa mwizi kaiba Sana tatizo CCM hawawezi kumpeleka mahakamani kwa sababu yeye pia anajua wana CCM wengi waliopita wamekula Sana nchi wezi hawawezi kumpeleka mwizi mwenzao mahakamani Alafu wadau tumieni akiri usimpende mtu kwa mapenzi yako Angalia atakuletea faida gani sio kumshangilia mtu amesha iba Sana nchi

    ReplyDelete
  5. unafiki tu. Mungu atawaona nyie mafisadi wakubwa mnaojificha nyuma ya Lowasa msionekane. Nashangaa mnafikiri kila mtu mjinga anawaamini. Watanzania hawakuwachagua mliiba kura bora mkae kimya

    ReplyDelete
  6. Meno ya tembo Zurich mbona kimyaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  7. na wewe ni alama ya shamba la bibi mmebebwabebwa tu... na kurisishana uongozi hamna kitu cha maana unachoweza ni kuropoka na kurudiarudia mada kama rowasa umeshamsema sana unafanya marudio tu,,, pole!

    ReplyDelete
  8. Na bado mkutano wenu mkuu Lowassa yumo akilini kwa wajumbe
    Pamoja na tumbua majipu
    Alikuwa kipenzi cha wengi ccm
    Ndo kila. Kukicha nape unazusha la kuzusha
    Na Mungu analipa wagonjwa wapo India
    Lowassa hupo masaki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad