PAUL Makonda Amtumbua Mhandisi wa Mkoa..Kisa Barabara Kujengwa Chini ya Kiwango

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemsimamisha kazi Mhandisi wa Mkoa, Josephat Shehemba kwa kushindwa kutimiza wajibu wake, ikiwemo usimamizi wa barabara na kusababisha kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema amefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi baada ya kuona injinia huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya usimamizi.

Alisema jukumu la usimamizi wa barabara, unapaswa kuwa chini ya Shehemba, lakini ameshindwa kufanya hivyo jambo lililosababisha usimamizi huo kufanya na wananchi na wakuu wa wilaya ambao sio kazi yao kufanya hivyo.

“Ni lazima alitakiwa kufanya kazi yake ya usimamizi na kuhakikisha barabara zinajengwa kwa kiwango kinachotakiwa lakini matokeo yake kazi yake ameiacha na kufanya na watu wengine ambao hawakupaswa kufanya hivyo,” alisema Makonda.

Aidha, Makonda alisema kukosekana kwa usimamizi mazuri wa kiongozi huyo kumesababisha barabara nyingi za mkoa huo kuwa chini ya kiwango na nyingine kuharibika muda mfupi baada tu ya kutengenezwa.

“Ameshindwa kusimamia lakini anakuwa mtu wa kwanza kudai fedha za kuwalipa wakandarasi ambao wamejenga barabara chini ya viwango angepaswa kusimamia atakapokwama au kumuona mkandarasi ameshindwa kufanya kazi yake kwa viwango basi angenieleza ili tuone tunafanya utaratibu gani,” alisisitiza.

Makonda pia alisema ni jukumu la kila kiongozi kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kuwa msimamizi mkuu katika idara yake.

“Hatutomvumilia kiongozi yeyote atakayekwenda kinyume na taratibu za kazi inavyomtaka kama ameshindwa bora ahame mkoa kwa sababu hapa kwangu sitamvumilia,” alisema.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hapa kazi tu safi sana kijana

    ReplyDelete
  2. Ndiyo Makonda huu ndiyo mwamko wetu wa sasa... Mchezo hatutaki maana yake hatukuona faida yake huko nyuma Hapa ni kazi tu.. tena kwa ufanisi wa hali ya juu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad