Paul Makonda Azishukia Kampuni za Ukandarasi wa Barabara Dar Kwa Kujenga Barabara Nyingi Chini ya Kiwango


SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam, imeifutia  kibali kampuni ya Ukandarasi ya Ishinomya  cha  kufanya ujenzi wa  barabara za halmshauri zote za jiji la Dar es Salaam kutokana kujenga barabara chini ya kiwango huku kampuni tatu zimetakiwa zisipewe zabuni mpaka pale watakapojiridhisha.

Akizungumza na waandishi habari jijini  Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kampuni zimekuwa ukandarasi zimekuwa zikifanya kazi chini ya kiwango ili barabara iharibike kwa ajili ya kupata zabuni nyingine.

Amesema kuwa hatuwezi kufika kwakuwa na barabara zenye kiwango cha chini  na kuendelea kuwepo kwa kampuni hizo ambazo zinajenga barabara chini ya kiwango na wanapofika mwisho nyuma zimeharibika.
Amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam barabara zina mashimo kutokana na kampuni kufanya kazi kwa mazoea.

Kampuni ambazo zimesimamishwa kufanya ukandarasi wa barabara mpaka wajiridhishe ni Germinex,  Delmonte  pamoja na Skol .
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam ndani ya mwezi mmoja kuwe hakuna barabara inayokuwa na mashimo na ni agizo  ambalo wanatakiwa kutekeleza.  
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huu ndiyo uwajibikaji tunao utegemea na kuutaka..hii itakomesha na kufupisha mazingira HEWA. ambayo ndiyo ulikuwa mfumo huko tulipotoka.. na tunasema kila mtendaji awe ni muamimifu na mtendaji mwenye ukweli ki nia na dhamira njema kwa nchi na qananchi..hongera makonda..hapa kazi tuu chini ya baba JPJM

    ReplyDelete
  2. huu ndiyo uwajibikaji tunao utegemea na kuutaka..hii itakomesha na kufupisha mazingira HEWA. ambayo ndiyo ulikuwa mfumo huko tulipotoka.. na tunasema kila mtendaji awe ni muamimifu na mtendaji mwenye ukweli ki nia na dhamira njema kwa nchi na qananchi..hongera makonda..hapa kazi tuu chini ya baba JPJM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad