Picha: Raymond wa ‘WCB’ Aringishia Mabunda ya Hela Instagram

Wakati mtaani raia wakilalamika kuhusu ukata wa hela toka Rais Magufuli aingie madarakani, mkali wa wimbo ‘Kwetu’ kutoka WCB, Raymond ‘Rayvanny’ ameamua kuringisha mabunda ya hela kupitia ukurasa wake wa instagram.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta kiki’ amepost picha kupitia instagram yake na kuandika jina la wimbo wake huyo, huku mashabiki wakitoa maoni yao juu ya wingi pesa hizo.

Raymond alisaini ‘WCB’ mapema mwaka huu kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi Tip Top Connection huku akiwa karibu zaidi na Madee.

Haya ni maoni ya mashabiki hao.

Tajibetese
Mmmmh @rayvannyy kama unatupenda fans wako hii ndo number yangu 0768046197 hata alfu kumi tuisogeze ramadhan

Blackgal_ake_dede
Hiyo kiki ndio yenyewe sio ya mademu fanya kunigawia basi ndugu @rayvanny

Am_coco_
That’s why I love you 😁,… Harmo abaki tu kwa mchaga, mi mpare nakutaka wewe .

Celinn1988
Watu wanavyojua kupangia watu kweny hela zao, mtadhani zenu mmefanyia kitu cha maana au mnaropoka tuu hapa.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. siyo mabunda yake ni ya kuringishia tu,hivi nyie wabongo ni rahisi kudanganywa namna hii hapo jamaa anatafuta kiki tu ameazima hayo mabunda kwa mtu ili watu wajue anazo kumbe hana, angekuwa anayo mabunda kama hayo unazani angebaki WCB si angekimbia aendelee na maisha yake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad