Picha zinatisha: Msichana wa Kazi za Ndani Achomwa na Moto Uarabuni

Msichana Mary Kibwana Kamango (pichani) raia wa Kenya ambaye alinyanyaswa na kujeruhiwa na mwajiri wake huko nchini Jordan amerejeshwa nyumbani.

Mary amesimulia kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa wasichana kutoka Afrika wanaofanya kazi za ndani katika nchi zilizopo katika Falme za Kiarabu.

Tukio lake lilihusisha kupigwa na mwajiri wake na kuchomwa kwa moto wa gesi mapema mwezi Aprili mwaka huu. Pamoja na kuomba msaada hakuna aliyemsaidia ikiwemo vyombo vya usalama nchini Jordan.

Baada ya tukio hilo la kusikitisha, raia wa Kenya wanaoishi katika nchini Jordan walichangishana fedha za nauli na kufanikiwa kumsafirisha mwenzao kurudi nyumbani. Kwa sasa Mary amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta ambako anapatiwa matibabu ya majeraha ya moto wa gesi.

Mary amewaasa wasichana wenzie dhidi ya unyanyasaji wanaofanyiwa wafanyakazi wa kazi za ndani katika nchi za Falme za Kiarabu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acheni kujiuza, kuiba,kunyanyasa na kuwatesa watoto wa waajiri wenu wakiwa makazini. kwani hata Africa case za hivi zipo nyingi sana, msiangalie ubaya upande mmoja tu haiwezekani mtu akuchome bila sababu. waschana wengi wa africa wakifika nchi za kiarabu wanaanza biashara ya kujiuza au kutoka na Waume za boss wao.... AFRICANS YOU NEED TO CHANGE(BADILIKENI)

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad