Picha:Uwoya Amtia Majaribuni Richie

Irene Uwoya na Richie.
WAKATI Waislam wakiwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya juzikati alimtia majaribuni msanii mwenzake Single Mtambalike ‘Richie’ walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar kulikokuwa na harusi ya mdogo wake Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Happy Mengere.

Kwenye ‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa amevalia kivazi kilichoacha mapaja yake wazi, alionekana mara kadhaa akimkumbatia Richie na hata paparazi wetu alipotaka kuwafutoa picha, staa huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu wakinong’ona chinichini.

“Uwoya hivi haoni anamtia mwenzake majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu analazimisha kupiga naye picha ya kumkumbatia, ila hawa wasanii wamezoeana sana,” alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa.

Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipojaribu kuwakaribia na kumuuliza Uwoya kulikoni anamfanyia mwenzake vituko alisema, alijisahau kuwa Richie yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila alipiga picha hiyo kama pozi la kawaida tu na wala hakuwa na nia mbaya.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nakumbuka sana enzi za Mr.Clean au wengine walimyita mzee ruksa ambaye yeye ndiye aliyekuwa rais wa awamu ya pili nchini Tanzania baada ya J.KNyerere ambaye aliitwa H.Mwinyi ilikuwa ni wakati kama huu wa mfungo wa Ramadhan badhi ya Waislam walilivamia bucha moja kule Manzese na kuvuruga vuruga ndani ya bucha kisa eti mwenye bucha alikuwa anauza nyama ya"FINE BOY"Au wenyeji humuita"KITI MOTO"ikawa balaa tupu vuta nikuvute ndipo mkuu wa nchi wa wakati huo aliponena kuwa hii ni nchi ambayo ina madhehebu mbalimbali ya dini na nchi huru kwa kila mtanzania na haki ya kuamini dini yeyote ile ili mradi mtu havunji sheria za nchi na pia akasema kama kuna watu wanakula nyama ya kiti moto wewe pia unaweza ukuchukua nyama ya mjusi pia ukala akamaanisha kuwa kila mtu yupo huru sasa hapo juu naona muhandishi wa habari analalamika kuwa huu ni mwezi wa Ramadhan huyo binti amepiga picha za nusu utupu kwanza jina la huyo binti linaonyesha kuwa yeye si wa madhehebu ya kiislam na pia hata kama jina lake lingekuwa la dhehebu hilo na yeye haamini hiyo dini yaani yeye yupo kama binadam lakini haamini dhehebu lolote wapo watu namna hiyo duniani pote je ingekuwaje?Au watu wanasahau kuwa nchi hii ina watu wa madhehebu tofauti na wapo wengine hawaamini katika dini yeyote ile kwa hiyo wasifanye mambo yao wayapendayo kwa ajili ya mwezi wa Ramadhan hata kama hawaabudu dhehebu hilo linalofunga Ramadhan?Nilifikiri Tanzania ni nchi ya democracy au?Nionavyo mimi ni sawa na ule masemo wa"MUWAMBA NGOMA HUVUTIA KWAKE"Kitu ambacho si haki na pia siyo ustaarabu inabidi sehemu zinazohusika zijaribu kuielimisha jamii ielewe vyema ili kuepuka hizi misunderstandings zinazojitokeza mara kwa mara kwani"USIPOZIBA UFA LEO KESHO UTAJENGA UKUTA"

    ReplyDelete
  2. Cha ajabu kitu gani
    Wote si waislam
    Hawakuwa msikitini
    Walikuwa kwenye harusi ya kikristo
    Tena ndani ya ukumbi
    Tanzania haina dini
    Ila watanzania ndo wenye dini
    Acheni bla bla bla kulazimisha ya mwaka 47
    Taifa linapata kodi kwa Sherehe hizo iwe za kiislam au kikristo
    Ramadhani isiwe kero kwa wasio waislam jamani

    ReplyDelete
  3. Mi huwa najiulizaga, ina maana hii miezi mingine watu wanaruhusiwa kuvaa, kuzini, kuiba, nk. kwa sababu sio mwezi mtukufu?

    ReplyDelete
  4. Mi huwa najiulizaga, ina maana hii miezi mingine watu wanaruhusiwa kukaa uchi, kuzini, kuiba, nk. kwa sababu sio mwezi mtukufu?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad