Polisi Dar es Salaam Wamng’ang’ania Zitto Kabwe

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema inaendelea na upelelezi kuhusu tuhuma zinazomkabili Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zitto ambaye ni Mbunge Kigoma Mjini na watakapokamilisha atafikishwa Mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema, sababu za kumhoji Zitto ni kutokana na kauli za uchochezi alizozitoa katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Zakhem, Mbagala.

Alisema, tayari Zitto ameshahojiwa katika kituo hicho mara mbili, lakini bado jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kujiridhisha dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Sirro alisema jeshi hilo haliwezi kuruhusu siasa ambazo zinavunja amani, hivyo ameendelea kuwataka wanasiasa kufuata taratibu na endapo wamekataza kufanya mikutano basi watii.

“Kama hakuna amani hakuna siasa hatuwezi na hatutakubali kuruhusu amani tuliyonayo itoweke sababu ya wanasiasa lazima kutii ili kulinda amani yetu,” alisema Sirro.

Hivi karibuni Zitto alijisalimisha Kituo cha Polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu baada ya kuandikiwa barua ya kuitwa kituoni na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Camilius Wambura.

Hatua ya Zitto kuhojiwa ilitokana na maudhui ya hotuba yake aliyoitoa Juni 5, mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Zakhem, Mbagala wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kutoka katika mahojiano hayo, Zitto alisema haoni kama hotuba aliyoitoa ina tatizo lolote, kwani hotuba hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kisiasa.

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Shida Salun, hembu mwambie huyu kijana apumzike anajipeleka kubaya Na akli Na busara Hana..na anasiriki kusema haoni ubaya wake..kweli Yuko timamu ???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Niambie wewe ameongea kipi kibaya?kuijadili bajeti?watanzania ndio maana mtaibiwa milele,kwani huyo raisi ni mungu?acheni hizo.

      Delete
    2. Kijana Zitto kabwe,kama ww ndio uko rais wa tanzania. kuusu bajeti ya nchi maskini iyo na kutegemeya misaada kutoka inje.Isitoshe watu awalipi kodi, lazima bajeti itakuwa ya kimaskini. Ongelea saana mambo ya kuwa na masomo na walimu wazuli ichini. Mengine yatakuja si kwa kuongelea sana bajeti.

      Delete
    3. Viongozi wengi wa Tanzania wana uwezo mdogo wa fikra na upeo mdogo wa kupambanua mambo kwa kina na ndio maana hawapendi changamoto za watu waliowazidi utashi na akili,wengi wanamchukia Zitto Kabwe usoni ila miyoni mwao wanatamani watoto wao wawe na utashi wa Zitto Kabwe.

      Delete
    4. Viongozi wengi wa Tanzania wana uwezo mdogo wa fikra na upeo mdogo wa kupambanua mambo kwa kina na ndio maana hawapendi changamoto za watu waliowazidi utashi na akili,wengi wanamchukia Zitto Kabwe usoni ila miyoni mwao wanatamani watoto wao wawe na utashi wa Zitto Kabwe.

      Delete
    5. Mdau, Mie naona huyu ni Punguani je we uko kama yeye au amekuzidi?? Manaake watu wanazidiana na kutofautiana. ama vipi?

      Delete
  2. ni kweli mdau akili zito hana kama kweli anazo angezingatia fujo analolitaka lianze mbona wanamchelewesha wamuake ndani au apelekwe mirembe apimwe mutapata proof kuwa huyu ni punguani wa akili

    ReplyDelete
  3. Si ndio zake WA kupotea Na kuinuka Mzee WA busala...bla bla nyi giiiiii ..tumekuchokaaaaaaa..rudi kwenu tuachie Amani ya nchi yetu..pungywani..haambiwi umepagawa umeota kuwa laisi mala mfalume..mala abunuwasi.. Mala Kalagosi..we Zitto unanini kilicho kusinu au kazi za watu!!????

    ReplyDelete
  4. Tena Ni Vizuri na Itakuwa ni somo jema na la nguvu kwa yeyote mwenye ni na lengo la kutuvurugia Amani na utulivu wetu na Nchi yetu.. Inawezekana wengine waka wanatumiwa na mabwana zao nje na ndani manaake maadui hawa sura tofauti japo ndani ya mioyo yao watakuwa na chuki na kuona katika nchi zao Wamekosa Amani na Utulivu.. Wanaona bora wawatumie ndani watu alio wapandikiza / Vibaraka kuwe kuthubutu kuwawezesha kufukia lengo lao la Uharibifu.. Tunasema Tanzania Yetu ni Nchi ya Amani na Watu wake Ni watulivu na Wamestaarabika Kiasi kuwa sisis tumekuwa watu wa kutolewa mifano kwa Uzuri wa Tabia Zetu na Nidhamu na Heshima katika Jamii za Ughaibuni popote alipo Mtanzania Mifano ni Mingi na ni mizuri tu. TANZANIA NI YA WATANZANIA NA KILA MMOJA WETU ANA JUKUMU LA KULINDA AMANI YETU/ YA NCHI YETU / YA WATU WETU / NA WATOTO ZETU... HATUTOMWACHIA MTU YEYOTE AU KIKUNDI CHECHOTE AU TAIFA LOLOTE KUWEZA KUTUINGILIA DIRECTLY AU INDIRECTLY KULETA UFISADI NA MVURUGO WA AMANI YETU NA NCHI YETU...SABABU TUNAYO / NIA TUNAYO NA UWEZO TUNAO...TUTAKEMEA / TUTAFUPISHA NA TUTAKOMESHA.. Wakati wowote mtu yeyote na mahali popote... Mungu ibariki Tanzania / Idumishe Amani yake na Upendo na Uzalendo.. na Mbariki Raisi wetu JPJM na Watendaji na Wawajibikaji wa Awamu yetu hii ya TANO

    ReplyDelete
  5. Unamuona Ocalan (Mkurdi) aliyekamatwa Nchini Kenya na Kupelekwa Uturuki... Hivi sasa Miaka nenda Miaka rudi hajahukumiwa ila wamemueka in isolation analindwa hana wa kumtembelea na sehemu aliyopo imepigwa marufuku Kuikaribia.. Sababu ni nini Amehamasisha watu na wengi wamepoteza maisha na inchi imeingia katika hasara kununua sila ili iweze kurudisha Amani na Utulivu.. wengi wamekuwa vilema / economy immesafa kwa vijitu vya upeo mdogo na uana siasa Uchwara kama huu... HUYU NI KUMFUNGA NA KAZI NGUMU mpaka hapo mungu atakapo mpa akili na kukua Kiakili...Hapa kazi TU

    ReplyDelete
  6. Hongera Sirro, Huyo msipomshughulikia sasa Atalipeleka Taifa kubaya ni mchochezi asiye na majukumu wala Uzalendo.. Mlimvizia kama alivyo dai na vibaraka wake kina Abdalah Hamisi na Mitemelwa au alijileta?? Hatua ya kumpeleka huko mbele ni Madhubuti na Sahihi ... Roha yake ni moja tu.... Shwain aliyekosa amani katika maisha na amejaa Uroho na Uchu wa Madalaka kwa jina la krasia.. Hapa kazi tu JPJM

    ReplyDelete
  7. Huyu nakumbuka siku zile Mbowe alimfanyia nini .. walimyanganya Simu zake na Laptop.. Halafu walitaka kunfanyizia... alafu ikawaje ikawaje...wakashiti.. sasa asijione labda atafanyiza kwa kutumiwa na maadui zetu.. Tunakwambia mwasiasa uchwara Rudi Kwenu na uwaambie kuwa Sikuweza na wala Sitoweza,... Watanzania Wako Imara na wanaipenda nchi Yao.. Ambayo kwa sasa iko chini ya watu Majasiri na shupavu kuitumikia na kuilinda katika ngazi zote... Mungu Ibariki Tanzania yetu na Watu Wake. na Raisi wetu JPJM....Na Serikali yetu ya Awamu yetu ya TANO katika kila ngazi..

    ReplyDelete
  8. Viongozi wengi wa Tanzania wana uwezo mdogo wa fikra na upeo mdogo wa kupambanua mambo kwa kina na ndio maana hawapendi changamoto za watu waliowazidi utashi na akili,wengi wanamchukia Zitto Kabwe usoni ila miyoni mwao wanatamani watoto wao wawe na utashi wa Zitto Kabwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Mie naona huyu ni Punguani je we uko kama yeye au amekuzidi??

      Delete
    2. Mdau, Mie naona huyu ni Punguani je we uko kama yeye au amekuzidi?? Manaake watu wanazidiana na kutofautiana. ama vipi?

      Delete
  9. Magufuli watumbue kweli Kweli.zitto ni kafisadi tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad