Polisi Wafunguka Minong’ono Kuwa Wanaipendelea CCM

Jeshi la Polisi limekanusha taarifa kuwa linakipendelea chama tawala cha CCM, bali limesema  litaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na kituo cha luninga cha  TBC usiku huu, Kamishna wa oparesheni na mafunzo wa Jeshi hilo, CP Nsato Marijani amesema Polisi ni taasisi inayofanya kazi kwa mujibu wa sheria bila kushinikizwa na mtu, watu au taasisi yoyote ile.

Amesema taarifa mbalimbali zimekuwa zikienezwa na watu wasio na uelewa kuhusu kazi za jeshi hilo kinyume na hali iliyopo.

“Polisi hatuko juu ya sheria na hata tunapofanya kazi tunakuwa makini ili kuepuka kukiuka miiko ya kazi yetu,” amesema.

Amesema jeshi hilo linaweza kushtakiwa Mahakamani kama litakuwa limetenda  kinyume cha Sheria.

“Kazi yetu ni kuhakikisha tunawalinda raia na mali zao, na hatuwezi kwenda kinyume na hapo.”

Amesema polisi hawezi kuua watu au kuwanyanyasa eti kwa lengo la kukipendelea chama tawala.

Amesema kile kinacho endelea katika Kisiwa cha Pemba, Zanzibar  kwa sasa, hakiwezi kufumbiwa macho na jeshi hilo kwani kinaashiria uvunjifu wa amani.

Kamishna Marijani amesema:

“Polisi hawawezi kukaa kimya pale wanapobaini mali za raia zinaharibiwa na kundi la watu fulani kwa makusudi, hiyo ni hujuma, lazima tufanye kazi ya kulinda mali hizo kama kanuni yetu inavyotutaka, kulinda usalama wa raia na mali zao.”


Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umtapiga saluti hadi akhera kwa wabunge

    ReplyDelete
  2. Mh!! tatizo ni mkate wa kila siku!!! sishangai kuelemea upande mmoja maana mmeshika makali lazima mtii amri ya mkuu...

    ReplyDelete
  3. yena hii ni maelezo kwatu wote..na ni lazima tuelewe hivyo na si vinginevyo..Jeshi letu kazi yake ni kulinda usalama na mali zetu..chochote kitakacho ashiria uvunjaji wa haya..Jeshi letu halitasita kaingia kati na kuhakikisha kwamba haya hayavurugwi. na mtu au kokundi chochote na wakati wowote na mahali popote na bila ya taarifa yoyote..Kwa hiyo mlijue hili kuwa hawangoji kukaeibishwa na hawato vumilia kuona Usalama wetu na Amani yetu iingie katika watu au vikundi vya watu na wao wanashangilia pembeni..Hawa ni wawajibikaji na wanayo hii dhamana kisheria na kanuni zeru zinathibitisha hilo..anaethubutu au kujaribu basi atashighulikiwa ipasavyo HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  4. yena hii ni maelezo kwatu wote..na ni lazima tuelewe hivyo na si vinginevyo..Jeshi letu kazi yake ni kulinda usalama na mali zetu..chochote kitakacho ashiria uvunjaji wa haya..Jeshi letu halitasita kaingia kati na kuhakikisha kwamba haya hayavurugwi. na mtu au kokundi chochote na wakati wowote na mahali popote na bila ya taarifa yoyote..Kwa hiyo mlijue hili kuwa hawangoji kukaeibishwa na hawato vumilia kuona Usalama wetu na Amani yetu iingie katika watu au vikundi vya watu na wao wanashangilia pembeni..Hawa ni wawajibikaji na wanayo hii dhamana kisheria na kanuni zeru zinathibitisha hilo..anaethubutu au kujaribu basi atashighulikiwa ipasavyo HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  5. Mbona wengi wsmeuawa, wengi wamechapwa nanyi, wengi vilema, mabomu, maji washa, bakora inanikumbusha enzi za ujerumani na waarabu. Inabidi mjitazame upya. Mjue sheria mpya na vyama vingi na si kutumwa na mwanachama mmoja kuvamia wengine, kupiga bakora watu kama mbwa, kutokujua mazingira mliyonayo na kusalimu amri kwa mkuu bila kueleza au kuuliza kwa nini mnaambiwa au mnatimwa hapo. Polisi aswe mnyanyasaji. Awe binadamu kabla ya kutenda jambo afikiri, aulize, adadisi. Nchi nyingine wanajirekodi wenyewe kwa ushahidi kama unabidi uende kortini.labda tununue mjirekodi kila kitu ili tupate ukweli zaidi wa mambo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad