Polisi Wamtia Mikononi Zitto Kabwe Wamhoji Kwa Dakika 90.....

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe  asubuhi ya leo June 13 2016 alikutana na wanahabari na kuzungumzia kuhusu polisi kuzuia kongamano ambalo liliandaliwa na chama hicho ili kujadili bajeti. Pia alizungumzia kuhusu yeye kusakwa na polisi kwa kuviziwa na sio kwa utaratibu wa wito.

Leo jioni  Zitto Kabwe alipokea wito wa kuhitajika Central polisi kwa mahojiano ambayo yalichukua zaidi ya dakika 90 .

Baada ya  kutoka kwenye mahojiano aliyepata nafasi ya kuzungumza ni wakili wa chama hicho Steven Mwakibolwa ambaye ameeleza sababu za wito huo kituoni hapo.

"Wamechukua maelezo ya Zitto kufuatana na kongamano la chama lililokuwa limezuiliwa jana.Baada ya mahojiano na mazungumzo na polisi, chama kitatoa taarifa rasmi juu ya nini kitafuta baada ya hapa." Amesema Mwakibolwa

"Kama alivyoeleza mwanasheria tumemaliza mahojiano na polisi kwa hiyo kesho tutatoa kauli yetu ya hatua inayofuata, nimeitwa polisi nimekuja, wanachama watulie tunaendelea na majadiliano na polisi ili tuendelee na kazi zetu za kisiasa kama kawaida" Amesema Zitto Kabwe

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mwana sasa Uchwara amekuwa "KIONGOZI MKUU"... Nyie watu wa Udaku mnatupotosha na vichwa vyenu vya habari!! aKIWA YEYE NI KIONGOZI MKUU ANAMUONGOZA NANI HUYO MCHANGANYIKIWAJI.. Au anaongoza wachanganyikiwa!! Kichwa kinatisha!! Au muhariri ni shemeji yake !! au Mjomba????

    ReplyDelete
  2. huna lolote fujo umezoea siasa sio yako wàachie wenyewe rudi kwenu tunahitaji amani

    ReplyDelete
  3. hivi kwa nini serikali inamzuia?inaonekan huyu raisi hajiamini,ana haki kikatiba,wapi demokrasia.?

    ReplyDelete
  4. Bwana Makongamano huyo ndio maana licha ya kuwa mbunge katika majimbo tofauti ya uchaguzi pale Kigoma. Bado Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa umasikini Tanzania. Sasa unajaribu kufikiria mtu kama huyu anakuwa Rais wa Nchi ndio basi tena imekula kwetu sisi Wananchi. Maana kila siku Nchi itakuwa inaongozwa kwa Mikutano ya Siasa na Makongamano yasiyoisha duh. Kaaaziii kwelikweli hahahahahahahaha huyoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo hahahahahahahahahaha

    ReplyDelete
  5. rais anawaogopa wapinzani kiasi cha kuzuia mpka kongamano nini hofu yake kama yeye kachaguliwa kihalali? nawashangaa bara na zanzibar hawana raha kwa wapinzani na wao ndio watawala wa mabavu udikteta ukizoea mtihani mtupu!!!!

    ReplyDelete
  6. rais anawaogopa wapinzani kiasi cha kuzuia mpka kongamano nini hofu yake kama yeye kachaguliwa kihalali? nawashangaa bara na zanzibar hawana raha kwa wapinzani na wao ndio watawala wa mabavu udikteta ukizoea mtihani mtupu!!!!

    ReplyDelete
  7. Yaani zito hizo nguvu unazozielekeza kwenye hayo makongamano,ungeelekeza na huku jimboni kwako.
    Mbona hatukuelewi?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad