PPFT : Gwajima Afutiwe usajili kwa kutoa kauli za uchochezi.


Ushirika wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT)umeiomba serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga amesema,kauli hizo zinaweza kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Askofu Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti huyo wa ppft amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwaa la kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na iliyopo madarakani.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtu si anapata maono kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, sasa inakuaje aonekane anafanya uchochezi!!? tuangalie tusije tukawa mafarisayo bila kujitambua!! huyu tumuache yeye na Pilato watajuana.

    ReplyDelete
  2. Mijitu mingine kujipendeza
    Afutiwe usajili kwa kosa lipi?
    Watanzania wengi ni wanafiki na waoga
    Aliyoyasema ni maoni yake
    Sisi kama jamiii tuchuje nakutafakari
    Kipi pumba au mchele
    Imekuwa kila kukicha uchochezi
    Fyuuuuu
    Tunaishi dunia ya utandawazi
    Tanzania nchi ya Amani
    Lugha moja
    Watu waseme
    Watanzania siyo wajinga
    Kusitokeeee kundi la watu wenye midomo kama kunguru weusi kujitia wanajuwa
    Tujibishane kwa hoja

    ReplyDelete
  3. Gwajima amesema ukweli. kila mtu anayo haki ya kuikosoa serikali. haogopwi mtu hapa nchi hii sio ya mtu mwenyewe ni mungu

    ReplyDelete
  4. Asante Askofu Pius Ikongo, Mawazo yako na Rai yako ni yakizalendo na inabidi tuliangalie hili suala .. Na vyama vyenye mielekeo na kauli au Dhana za uchochezi na uvurugaji.. Wasipewe nafasi katika Tanzania yetu ya Amani na Usalama na pia tunavyo vyombo vya Dola vinavyohusika na Usalama pia tungeomba wawashughulikie wote wenye Nia hizi za kuvunja Amani nchini kwetu. Mungu ibariki Tanzania yetu na udumishe Amani na Usalama...

    ReplyDelete
  5. miaka hii tutaona wanafiki wengi na tutasikia pumba nyingi sana kisa asili ya uoga

    ReplyDelete
  6. Mungu apishie mbali wabongo hamjawahi kuiona madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe(civil war)msipime kabisa mnasomaga magazetini au kusikia kupitia luninga nini kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za jirani zenye matatizo ya kisiasa na kuamua kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe mimi niliwahi kushuhudia kwa macho yangu wakati huo nchini Msumbiji vita iliyodumu takribani miaka 13 hivi siyo mzaa kwa hiyo huo usemi wa sisi wabongo siyo waoga si kweli kabisa kila binadamu lazima awe na uoga hasa kama yatokeapo machafuko nchini kwake tuombe iendelee amani upendo na umoja bongo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad