Rais Magufuli Aanza Kubanwa

RAIS John Magufuli ametakiwa kutangaza rasmi tarehe na namna ya kurejea kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya ili kukamilisha hatua zilizobaki, anaandika Pendo Omary.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) katika mkutano maalum na waandishi wa habari.

Deusi Kibamba, Mwenyekiti wa JUKATA amesema, tathimini jumala ya taasisi hiyo mebaini kwamba, mchakato umeshidwa kujenga muafaka wa kitaifa unaohitajika kama za la mchakato wa katiba na hivyo kupelekea katiba inayopendfekezwa kuwa na kiwango duni cha maridhiano ya kitaifa.

“Kwa hapa tulipo, mchakato wa Katiba unahitaji nguvu ya ziada ili uanze mapema katika mwaka wa fedha unaoanza wiki mbili zijazo kwa sababu mchakato haukuahirishwa kisheria kwa mtindo wa tangazo la serikali kabala ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Pia, zaidi ya kugusiwa na Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa Bunge mwishoni mwa mwaka 2015, haijaonekana nia wala dalili za serikali kutaka kurejesha mchakato wa katiba mpya. Ndio maana JUKATA tunaungana na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa katika hoja kuwa mjadala wa kitaifa unahitajika sasa,” amesema Kibamba na kuongeza;

“Bila Katiba Mpya yenye misingi imara ya utawala bora utumbuaji majipu na ‘hapa kazi tu’ inaweza kuwa kauli mbiu zisizoeleweka kwa Watanzania kwa kukosekana misingi imara ya kikatiba na sheria wa utekelezaji wake.

Kibamba amesema, namna utumbuaji majipu unavyofanyika wakati mwingine unaonekana kuvunja heshima, utu na faragha ya binadamu pamoja na misingi mikuu ya haki za binadamu kwa mujibu wa Katiba.

Aidha, JUKATA limeitaka serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka bungeni miswada ya kurekebisha sheria zinazosimamia mchakato wa wa katiba kwa ajili ya kuzihuisha katika tarehe zake zote zilizopitwa na wakati.

Hatua hiyo inatokana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na ile ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013 kupitwa na wakati na haziwezi kutumika tena bila marekebisho, bunge la bajeti kuelekea kumalizika bila miswada wa marekebisho ya sheria hizo kupelekwa bungeni na hakuna bajeti iliyotengwa katika suala la katiba kwa mwaka wa fedha 2016/2017

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hilo Ni suala ambalo nadhani mdau hapo huu Na walioshiriku Huko jukwaani JUKATA..KINA KIBAMBA NA KAMA KINA KIBAMBA..NI Kwamba wameshindwa kuelewa changamoto zilizokuwapo mpaka mchakato inafika ulipofika..na hii kwa sasa hivi Na awamu yetu hii ya Tano tunavyo vipaumbele ambacho tumeshavipangia strategies Na priority Na Hilo Ni suala ambalo tutalichukulia as the time permit..Kwa sasa hivi Na serikali yetu hii..hatukulipangia katika vipaymbele vyetu..sema tutashauriana Na Kama itawezekana tutalijadili Na kuangalia njia ya kuweza kulifanyua kazi..sema naoenda kuwataarifu very transparently Hilo siyo moja ya current priorities ila tuyaliangalia..Hapa kazi iko pale pale Na asiyee kewa Tuko tayari kumuelimisha..kwa hiyo tunaomba uvumulivu Na uzalendo wenu WA hali yya juu..michakato inayo wakabili wananchi Ni mingi Na our priorities Ni kuomdoa Na kuzishughulika matatizo yanayo mkabili Mtanzania kila siku rather than making Inks on paper..wakati WA hewa umeshapitwa Na we are focused on more beneficial activities to revamp the corrupted system which we have inherited...HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. Pendo Omary..umejitahidi..ila kichea cha habari hakiendani Na maudhui ya habari..labda ningekusaidia..nionavyo Mimi ingeamdia ..JUKATA WAOMBA MCHAKATO WA KTIBA UANGALIWE UPYA/USHUGHULIKIWE ULIPOFIKIA..hapo nadhani ingeleta mantiki..Utashi katika uandishi jua unaandikia Taifa..we need to be sensible Na responsible reporter's and more professional approach..Hapa Kazi tu

    ReplyDelete
  3. Umeanza RAISI MAGUFULI AMETAKIWA ( Ametakiwa Na nani?) Nani anae uwezo WA kumpa Raisi wetu Ultimatum..PENDO..Be neutral 😐 and professional ethics when reporting..Umepotosha yote with a wrong 👎 start..JAEIBU TENA MARA NYINGINE...Hapa kazi Tu..

    ReplyDelete
  4. Kwanza kama alvyosema msemaji alipita hapo juu ni nani ana mamlaka ya KUMTAKA RAIS AFNYE JAMBO FULANI? Kibamaba hana ubavu huo labda naona kiswahili kinakuwa kigumu na kinashindikana vipi sasa kiingerza? acha kutoa taarifa kwa umma zenye ukakasi na zisiszoelweka. Kumtaka mtu ni kumpa amri na huyo unayempa amri hiyo hana jinsi lazima afanye, hii imezoeleka kwenye majeshi yetu. Uandishi tunasomea wapi au tunatumika? acheni BIASNESS nyinyi ni kwa ajili ya umma na si kwa manufaa ya vyama na watu wenye fedha huku mkiwa mbele kuipotosha jamii ya watanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad