Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia jana.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Rais amemteua Dk Charles Mlingwa ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha kujaza nafasi hiyo.
Mulongo anakuwa mkuu wa mkoa wa pili kutimuliwa kazi na Rais Magufuli baada ya Anne Kilango Malecela aliyekuwa Shinyanga.
Hata hivyo, tofauti na Kilango ambaye alitimuliwa kutokana na kutoa taarifa potofu kuhusu watumishi hewa mkoani mwake, Ikulu haikutoa sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Mulongo.
Mulongo ameondolewa madarakani miezi sita baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk Faisal Issa baada ya kutofautiana na Mulongo wakati huo akiwa mkuu wa mkoa huo.
Baada ya kumwondoa Dk Issa na nafasi yake kujazwa na aliyekuwa Kamishna wa Polisi, Fedha na Utawala (CP) Clodwig Mtweve, miezi miwili baadaye Rais alimbadilisha Mulongo kituo cha kazi akimhamishia Mara.
Alipoulizwa jana jinsi alivyoipokea hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi yake Mulongo alisema: “Sina taarifa rasmi.”
Kabla kuhamishiwa Mara akitokea Mwanza, Mulongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Alishika nafasi hiyo baada ya kupandishwa cheo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.
Mwenzako akinyolewa - nawe jiandae huyu RC kiukweli alimufedhehesha swahiba wangu Dkt. Faisal Issa kwa ubabe usiokuwa na maana. Sasa iwapo kuachishwa kazi ni kuzuri ngoja kwa muda huu naye aonje kikombe hicho
ReplyDeleteWaandishi naomba kutoa
ReplyDeleteHoja kuna tofauti gani ya kutengua na kufanya mabadiliko ya viongozi
Yeh ! useme wewe kiazi , nikisema mimi Muhogo naambiwa nina mizizi ,
Deletehumu kiswahili kibovu sana , halafu wanawacheka Wakenya
Wakati mmoja ....niliona Superwoman wa Wanawake ...Rejea taarifa ya Joyce Kiria hapo kando
Wakati mwingine hufikiria hawakwenda shule ya Uwandishi au Lugha inawapiga chenga .....
Hawaelewi hawajitambui , hata kutengua na kufanya mabadiliko hawakujui
Ahsante Anony 10.09 AM
HOJA IMEPITA NA IMEUNGWA MKONO
ReplyDeleteKutenguliwa ni sawa kufukuzwa kazi?
ReplyDeleteAu anabakia kwenye ajira mshahara wa bure hadi upangiwe kazi nyingine ?
Bana matumuzi hiyo