RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli ameliagiza jeshi la Polisi kutumia mbinu za kisasa katika kukabiliana na uhalifu na kuifanya nchi kuwa sehemu salama nyakati zote.
Dk Magufuli ameonesha kushangazwa na askari wa Jeshi la Polisi kunyang’anywa silaha yake na majambazi na wakati mwingine kuuliwa na majambazi, akihoji uwezo wa majambazi kiasi cha kuwatesa polisi kiasi hicho.
Rais alikuwa akizindua Mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao, ambao una dhamira ya kupunguza uhalifu ambapo ameliagiza jeshi hilo kuwahi kushughulikia majambazi kabla ya wenyewe kushughulikiwa na majambazi hayo.
Amesema kama ni silaha polisi wanazo, mafunzo wanayo lakini wanazidiwa na majambazi hadi kunyang’anywa silaha kwanini? Pia Rais amelitaka jeshi hilo kuwashughulikia baadhi ya askari wake ambao hawana nia njema na jeshi hilo.
Awali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu alisema mpango huo unalenga katika maeneo manne akiyataja kuwa ni Kuboresha mbinu za kupambana na wahalifu na majambazi kwa kuwa na vituo vya polisi vya kuhamahama na kutumia mfumo wa kisasa wa GPS katika doria za jeshi hilo.
Pili, Mangu alisema ni kuongeza ubora wa huduma katika vituo vya polisi ambapo polisi watakuwa wanatatua na kusikiliza kero za wananchi kwa haraka zaidi na kwa muda mfupi sana.
Tatu ni kuboresha mawasiliano ndani ya jeshi la polisi pamoja na jamii. Katika hili IGP Mangu anasema watasaidiwa na mfumo wa GPS katika kuwajua wananchi wanaosumbua jeshi la Plosi kwa kupiga simu za uongo na zenye lengo ovu.
Nne mpango huu wa kuboresha usalama unalenga katika kubaini vyanzo vya fedha kwa jeshi hilo kwa matumizi mbalimbali ndani na nje ya jeshi hilo.
Watendaji na Makamanda wa Jeshi letu la Polisi kuanzia ngazi ya Chini kabisa katika Vikosi vya Usalama .. Tunawaaminini na Jukumu tumekupeni Uendaji na Utekelezaji wa Usalama ni Jukumu letu sisi sote wananchi. Ajili anaemdhuru (Jambazi) mwananchi ni Mwananchi mwenzake aliye amua kujitafutia maisha kwa njia ya urahisi na bila kujali kuwa Kumdhuru mwenzake kwa lengo la kujipatia mali kiharamu kwako siyo tatizo na Hajali. Sasa huyu anakuwa si mwenzetu katika Jamii yetu. Na tusimruhusu wala kumuonea huruma!! Ni bora tumuondoe haraka sana katika kazi yake hii batili na katika Jamii manake yeye amuamua kuwa mvunja Amani na Usalama... Ni Imani yetu mmejipanga na Huu Usumbufu katika Jamii zetu Tutautokomeza kabisa. Nia yenu kwetu ni nzuri / Uwezo wenu ni Mzuri na Tunauamini na Ushirikiano wetu kwenu nyinyi na Vyombo vyote husika Tutakupeni ili Kulikabili hili tatizo ambalo nyinyi na sisi wote HATULIPENDI NA TUMELIKATAA... Mungu zidi kulipa Ujasiri Jeshi letu la Usalama na Kuendelea Kulibariki Taifa letu kuwa na Amani na Usalama wakati wote.. Na hatutomruhusu Mtu / Kikundi au Watu wenye nia na Lengo La kutuvurugia Amani na Usalama wet..Mungu ibariki nachi yetu na Viongozi na watu Wake.
ReplyDeleteWatendaji na Makamanda wa Jeshi letu la Polisi kuanzia ngazi ya Chini kabisa katika Vikosi vya Usalama .. Tunawaaminini na Jukumu tumekupeni Uendaji na Utekelezaji wa Usalama ni Jukumu letu sisi sote wananchi. Ajili anaemdhuru (Jambazi) mwananchi ni Mwananchi mwenzake aliye amua kujitafutia maisha kwa njia ya urahisi na bila kujali kuwa Kumdhuru mwenzake kwa lengo la kujipatia mali kiharamu kwako siyo tatizo na Hajali. Sasa huyu anakuwa si mwenzetu katika Jamii yetu. Na tusimruhusu wala kumuonea huruma!! Ni bora tumuondoe haraka sana katika kazi yake hii batili na katika Jamii manake yeye amuamua kuwa mvunja Amani na Usalama... Ni Imani yetu mmejipanga na Huu Usumbufu katika Jamii zetu Tutautokomeza kabisa. Nia yenu kwetu ni nzuri / Uwezo wenu ni Mzuri na Tunauamini na Ushirikiano wetu kwenu nyinyi na Vyombo vyote husika Tutakupeni ili Kulikabili hili tatizo ambalo nyinyi na sisi wote HATULIPENDI NA TUMELIKATAA... Mungu zidi kulipa Ujasiri Jeshi letu la Usalama na Kuendelea Kulibariki Taifa letu kuwa na Amani na Usalama wakati wote.. Na hatutomruhusu Mtu / Kikundi au Watu wenye nia na Lengo La kutuvurugia Amani na Usalama wet..Mungu ibariki nachi yetu na Viongozi na watu Wake.
ReplyDelete