Rama D Afunguka Kuhusu Yeye na Lady Jay Dee

Mwanamuziki wa R&B nchini Tanzania Rama D, amekanusha vikali habari zilizotapakaa mtandaoni kwamba kwa sasa anatoka kimapenzi na mwanadada Lady Jay Dee, amesema wanaheshimiana sana na haiwezi kutokea kitu kama hicho daima .

Hata hvyo Rama D ameendelea kusema kwamba yeye anamfaham mpaka mpenzi wa mwanadada Lady Jay Dee na kusema hata siku ya show ya ‘Naamka Tena Concert’ alipanda jukwaani kuonesha jinsi anavyomkubali mwana dada huyo.

Rama D anasema anawashangaa sana watu wanaoenda kufanya video zao nje na kusema kwamba haoni sababu ya kufanya video hizo nje kwani hapa nyumbani kuna mazingira ya kutosha kufanya video nzuri zitakazoitangaza nchi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad