Serikali: Hakuna Nafasi ya Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Kubadili Mchepuo au Shule

SERIKALI imesema shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, zimejaa hivyo hakuna nafasi ya mwanafunzi kubadilishiwa shule au mchepuo aliochagua.

Hayo yalibanishwa jana katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari mjini hapa na Msemaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Rebecca Kwandu.

Kwandu alisema baada ya serikali kutangaza wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano, baadhi ya wazazi na wanafunzi wamekuwa wakifika ofisi za Tamisemi kuomba kubadilishiwa shule au tahasusi (michepuo) walizochaguliwa.

“Tunapenda kuwaarifu kwamba shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2016 zimejaza, hivyo hakuna kinachoweza kubadilishwa,” alisema Kwandu.

Aidha, Kwandu alisema vigezo ambavyo vilitumika katika uchaguzi huo ni pamoja na ufaulu na uchaguzi wa wanafunzi wenyewe juu ya masomo wanayopenda kuendelea nayo kidato cha tano na sita.

“Kulingana na utaratibu uliowekwa na serikali, mwanafunzi mwenye sifa za kuchaguliwa kuendelea kidato cha tano na vyuo vya ufundi ni yule ambaye ufaulu wake ni kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu. Wanafunzi hao wamepangwa kulingana na ufaulu wao masomo waliyochagua na nafasi zilizopo,” alisisitiza.

Pia alisema nafasi za shule walizopangiwa wanafunzi zimezingatia miundombinu ya shule husika na uwezo, na kwamba kila shule imepewa wanafunzi kulingana na nafasi zilizopo, hivyo hakutakuwa na nafasi ya kuwabadilisha kutoka shule moja kwenda nyingine kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kuripoti katika shule na vyuo walivyopangiwa kama walivyoelekezwa.

Alisema mwanafunzi ambaye hataripoti ifikapo Julai 24, ambayo ni tarehe ya mwisho kwa muda uliopangwa, atakuwa amepoteza nafasi yake kwa kuwa itachukuliwa na mwanafunzi mwingine ambaye hakupata nafasi awali.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. It's not fear
    Ndo tunapata watu vilaza
    Kusomea taaluma ni uamuzie wa msomaji
    Poleni msomao wenye pesa someni nje
    Kila mahali jamani

    ReplyDelete
  2. Ni kweli wazazi wanaheshimu maamuzi ya mh, waziri wa Elimu, lakini lazima muangalie jinsi walivyopanga Tahasusi za watoto hao. Mfano mwanafunzi kafaulu masomo ya sayansi vizuri, imkuwaje anapangwa kwenda masomo ya arts?mfano HGL? inashindikana kupangwa CBG, PCB au PCM.Wanasayansi ilismwa na wizara kuwa niwachache lakini kwa hali hii inaonekana serikali haiwahitaji wanasayansi. Nilimuomba mhe, waziri kuanagalia upya namna walivyopangwa watoto ili kuona namna ya kufanya ili kulikomboa taifa katika kukoskana kwa wanasayansi. Wasiwasi wangu ni kuwa uenda wanafunzi wengi hawaenda shule walizopangiwa kwa sababu watoto hao na wazazi wamkatishwa tamaa na upangaji huo. Pia mimi naona ingetolewa fursa kwa wazazi na wanafunzi wao kuomba kubadilishiwa mchepuo kulingana na walivyofaulu na kupenda masomo ya sayansi na ndiyo maana walifaulu. Wazazi wanaombwa kusikilizwa kuhusu jambo hili badala ya kuweka utaratibu mgumu ambao siyo rafiki na wazazi na wanafunzi wenyewe, kwani nia ni kupata wataalamu watakao isaidia nchi yetu hapo baadae.Hili ni ombi kwa Mh, Waziri wa Elimu.

    ReplyDelete
  3. Kweli hata sisis wazazi bado tuna sisitiza ombi la kubadilishwa tahasusi kwani mwanafunzi mwenyewe kashinda vizuri masomo ya sayansi na anayapenda ivo inakuwaje asisaidiwe?.

    ReplyDelete
  4. Kweli hata sisis wazazi bado tuna sisitiza ombi la kubadilishwa tahasusi kwani mwanafunzi mwenyewe kashinda vizuri masomo ya sayansi na anayapenda ivo inakuwaje asisaidiwe?.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad