Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma nzito za serikali ya Kenya, rais Magufuli asaidiwe kidiplomasia

Serikali ya Tanzania sasa itoke hadharani kujibu Tuhuma za Serikali ya Kenya na viongozi wa Muungano wa JUBILEE kuwa Rais Magufuli anamdhamini kifedha Kiongozi wa Upinzani Raila Amolo Odinga kusababisha Maandamano, ghasia na hatimaye kuipindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

Siku Chache Zilizopita Msemaji wa Serikali ya Kenya Erick Kiraithe alisema kuwa tayari kuna taarifa za kijasusi kuwa kuna wanasiasa nchini Kenya wanadhaminiwa na kusaidiwa na Nchi Mbili Jirani maadui wa Kenya kutaka kuvuruga amani na kuiangusha Serikali na kudai kuwa Baraza la Ushauri la Usalama (National Security Advisory Council) lilikutana siku ya Jumatatu kuangalia namna ya kuwashughulikia watu hao

Mbunge wa Jimbo la Starehe Mwenye ushawishi ndani ya Serikali ya JUBILEE akiambatana na wabunge wengine alifanya mkutano na waandishi wa Habari Nairobi Hoteli na Kuwataja marais John Magufuli wa Tanzania na Salva Kiir wa Sudan ya Kusini

Rais Magufuli akiwa mapumzikoni CHATO msimu wa Sikukuu ya Pasaka alikua Mwenyeji wa Raila Odinga anayejiandaa na Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2017

Pia Mwezi Desemba nilialikwa na Mwenyekiti wa Vijana wa ODM wakati huo Rashid Mohammed n kwenye mkutano mkuu wa chama cha ODM kumteua Mgombea Urais 2012 nchini Kenya.Mhe.Magufuli pia alikuwepo. Nilimshuhudia Mhe.Magufuli akiwa waziri wakati huo akidai amehudhuria mkutano ule na kutangaza kuwa Raila Odinga ni Rafiki yake na amekuja kumuunga Mkono.Aliendelea kushtua watu Ukumbini akidai kwamba wagombea wengine wanaotarajia kuchuana na Raila Odinga hawawezi kusafiri hata nje ya nchi.Kipindi Hicho Uhuru Kenyatta na Willium Ruto walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mahakama ya kimataifa ya ICC.

Mhe.Magufuli akaendelea kusema hata Odinga angegombea jimbo la Chato yeye Magufuli asingethubutu kugombea maana asingeweza kumshinda

Urafiki binafsi wa Raila Odinga na Rais Magufuli sio tatizo jwani hata Mwalimu Nyerere alikua na urafiki na akina Thom Mboya,Jaramogi Oginga Odinga ila tatizo ni pale ambapo Mhe.Magufuli anaposhindwa kuwa senstive kisiasa na Kidiplomasia.Mbaya zaidi tuhuma zinatolewa na serikali ya nchi jirani tena mwanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Rais Magufuli anatumia Raslimali za nchi kumfadhili Mpinzani wa nchi jirani kwa lengo la kupindua serikali kwa sababu ya urafiki wao tu

Nikumbushie tu kitendo alichofanya Mhe.Magufuli kipindi kile nilisema na niliandika kuwa kitakuja kuleta matatizo ya kidiplomasia siku za usoni ikiwa ODM wangeshindwa kwani tayari kupitia Udhaifu alioonyesha waziri wa serikali ya Tanzania Mhe.Magufuli wakati Ule walishaaminisha Umma kuwa serikali ya Tanzania inawaunga Mkono.Kosa hili la Kidiplomasia ameendelea kulirudia.

Rais Jakaya Kikwete alikuwa Rafiki wa Kalonzo Musyoka lakini Uhusiano wao haujawahi kuibua mgogoro wa kidiplomasia na au kutoaminiana baina ya serikali hizi mbili

Tuhuma hizi ni nzito na zinazochochea mgawanyiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kitendo cha Serikali ya Tanzania kukaa kimya hadi muda huu maana yake kinatoa Silent Consent kuwa nu kweli hasa msemaji wa Serikali anaposema kwa ujasiri kuwa serikali yao ina taarifa rasmi

Mwaka 2013 kulikua na mgogoro wa kidiplomasia uliotishia kuipasua Jumuiya ya Afrika Mashariki .Kenya,Uganda na Rwanda ziliunda Muungano wao wa hiyari (Coalition of The Willing-CoW).Jitihada kubwa za kidiplomasia zilifanyika

Sasa muda huu Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa Mashariki na Tanzania kama Mwenyekiti hatupaswi kuwa chanzo cha migogoro ndani ya jumuiya kwani sisi ndio tunaopaswa kuonyesha uongozi katika Diplomasia kuhakikisha Malengo ya Mtangamano(Intergration) yanafikiwa.

Jitihada zozote za Serikali ya Tanzania na wapambe wake kutumia propaganda pengine kwa kuibua hoja ya Bomba la mafuta Kutoka Uganda na Kupita Tanzania badala ya Kenya na Suala la Reli ya Rwanda kwamba ndio limesababisha wivu itakua ni uamuzi mbaya kidiplomasia

Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma hizi kama si kweli basi Serikali ya Kenya iombe Radhi

Kenya na Tanzania zinahitajiana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote kiuchumi

Katika tathmini iliyotolewa bungeni jana,biashara ya Kenya na Tanzania imechangia sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi hizi

Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao ni wanadiplomasia Maahiri Dr.Augustine Mahiga wa Tanzania na Amina Mohammed Jibril wa Kenya wasaidie kunusuru hali hii ambayo inahatarisha Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizi Mbili

Na Pia Rais Magufuli asaidiwe ili apate uzoefu wa Kidiplomasia katika maneno na matendo yake.

Kwa mfano kitendo cha kuongea na Rais Kenyatta mwezi March walipokutana Arusha na kuahidi kusaidiana kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili na kisha mwezi mmoja baadae kumwalika Raila Odinga akiwa Mapumzikoni(Inaweza kutafsiriwa alichukua likizo ili akutane na Odinga isionekane amekutana nae ikulu) hakikutoa gesture nzuri kidiplomasia

Wakati Rais Magufuli anahutubia mkutano wa mfuko wa Wafanyabiashara Mwezi Desemba 2015 aliitaja kampuni ya Broakside Dairy Limited kuwa ilikua ikifanya biashara kiadui na kinyume na misingi ya Biashara nchini.Kampuni hiyo ilimilikiwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.Kidiplomasia Rais hakupaswa kutamka na kuitaja kamapuni ile bali angeweza kukwepa na kutumia namna nyingine au mtu mwingine kama ilikua ni lazima itamkwe.Siitetei kampuni ile isipokua ni udhaifu mkubwa wa kidiplomasia aliouonyesha Rais ingawa anaweza kujitetea kuwa alikua anasimamia Sheria.Diplomasia ni namna ya kumwambia mtu kafie mbali na yeye akakuuliza mbali kiasi gani badala ya kukukasirikia.Rais anapaswa ajifunze hili

Sasa hizi tuhuma za serikali ya Kenya na viongozi waandamizi zijibiwe na kama si kweli serikali ya Kenya Iombe Radhi.

Kama ni kweli inawezenaje Wanachi wa Tanzania wakose Sukari halafu Rais afadhali shughuli kama hizo nchi jirani?Na iweje sasa Serikali yake izuie mikutano ya kisiasa nchini?

Aluta Continua,Victory Ascerta......

Ben Saanane

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hv ww muandishi yani nataman nikutolee neno chafuuuu kwa akili kabisaa unadhan mh.Rais anaweza kufadhili sijui kupindua wat so ever kabisaa wakati unamuona raisi navyohangaika na hii nchi nchini kwakwe kwenyewe kuna matatizo ndo akamfadhili rafiki yake mi naamin kukutana kwao ni kwa ajili ya kuongea mambo yao binafs na kupeana ushauri hata kama ni rafiki yake mkubwa vip hawezi kufanya kitu kama hicho mh.raisi hajafikia huko plzz hz propagand zinazoenezwa juu yake zikomeshwe hao ni maadui tu wanaotaka kumchafua sababu wanaona utumishi wake ni umetukuka..watu wanazua tu vitu..na kibaya mh Rais huwa yupo straight hakwepeshi hana kona kona anasema ukweli hzi sio zama za kuoneana haya bwana ooh nikisema hv nitaharibu uhusiano...uhusiano upi?acheni mambo ya kipuuzi kuzusha tuhuma za kijinga kabisa...mm sio ccm lakn mengine mtu una macho unaona mnajaribu kila njia kumchafua Raisi its not guuud acheni mnaboa...

    ReplyDelete
  2. Wasomi wana msemo wao,no research no right to say je wewe ulieandika mada hii umefanya uchunguzi WA kutosha,ushahidi upo wapi au umeongozwa na mtazamo yako. Tuthibitishie hayo usemacho. Raisi hata mwaka bado ingependeza mkashauri kwa maendelea ya taifa letu sio kuangalia mapungufu unataka niambia wewe siku zote upo sahihi katika kila Jambo ufanyalo mbona tunakuwa wepesi kuhukumu bila kujiangalia sisi kama sisi tumefanya nini kwaajili ya serikali.

    ReplyDelete
  3. wewe ulie andika hizi abari akili yako iko sawa kweli

    ReplyDelete
  4. Mngejua wananchi hasa vijijini hawataki propaganda za siasa Bali wanataka MTU anayejua matatizo yao na namna ya kuondoa ukiangalia kama sehemu kubwa zilizokuwa zinashikiliwa na wapinzani zimechukuliwa na ccm,mfano kigoma wanangu waliangalia umefanyanini kutatua changamoto zinazowakabili kama Maji,nahuduma zote zajamii ambazo zinawakumba moja kwa moja sio makelele bungeni,na ndo maana watu wanamwamin rahisi kwaajili hiyo hata kama mnajitahidi kumwalibia. Tunataka vitendo vionekane

    ReplyDelete
  5. Ben Saanane na Udaku na wote yenye fikira za kuandika haya. Hili Mlio andika na Jinsi mlivyo andika kutokana na Mwangalio na Upeo wa Ushabiki uliojificha ndani yake.. Tunakwambia na tunawambia... Kama mmetumwa au unajaribu kuona Sisi tutajibu ni au Mtukufu Raisi JPJM atajibu au atoe maelezo... Tunakwambia kuwa Haya hayapo na wala yatakuwepo na Hakuna Yeyote wa Ngazi yeyote atakaejibu. Hayako wala hayatokuwepo na majirani zetu tuko nao vizuri na wewe kama unatumiwa karibu tutakumuria na ikibidi tutakutumbua ipasavyo.. Na ufupishe habari za Dizaini hii. Ajili haijengi Tija wa Hoja wala mahusiano mema na majirani zetu ambayo kila nchi mojawapo inahitaji Uhusiano na ujirani mwema...umejaribu na umepotea step ...mahusiano yetu ni mazuri na yanazidi kunawiri chini ya Uhuru na JP...

    ReplyDelete
  6. Ben Saanane na Udaku na wote yenye fikira za kuandika haya. Hili Mlio andika na Jinsi mlivyo andika kutokana na Mwangalio na Upeo wa Ushabiki uliojificha ndani yake.. Tunakwambia na tunawambia... Kama mmetumwa au unajaribu kuona Sisi tutajibu ni au Mtukufu Raisi JPJM atajibu au atoe maelezo... Tunakwambia kuwa Haya hayapo na wala yatakuwepo na Hakuna Yeyote wa Ngazi yeyote atakaejibu. Hayako wala hayatokuwepo na majirani zetu tuko nao vizuri na wewe kama unatumiwa karibu tutakumuria na ikibidi tutakutumbua ipasavyo.. Na ufupishe habari za Dizaini hii. Ajili haijengi Tija wa Hoja wala mahusiano mema na majirani zetu ambayo kila nchi mojawapo inahitaji Uhusiano na ujirani mwema...umejaribu na umepotea step ...mahusiano yetu ni mazuri na yanazidi kunawiri chini ya Uhuru na JPJM...

    ReplyDelete
  7. Kama Humjui Magu (JPJM), Pole sana... Magu tumemuamini na Tumempa nchi ili aweze Kutuvusha na Kuiongoza Safari yetu ya Maendeleo.. Kazi ni Ngumu na Amekubali kuchukua hii heshima tuliompa katika wakati Mugumu wa kila sehemu Hewa..Hewa.. Sasa kwa Taarifa yako mwandishi na waliokutuma na wanao kutumia tunakwambieni .. KICHWA CHA HABARI NA MAUDHUI YAKE .. NI choko choko isiyo na Mashiko na Msukumo unaonekana unachembe chembe za Chama na Chuki binafsi... Nisicho kijua kuhusu we mwandishi dhamira yako na Lengo lako?? Kumbuka na Ujue Mtukufu Raisi JPJM na Sisi hatutetereki wala kujibu katika Gazeti wala hapa Uppuzi wako na Usirudie tena kutuwekea Upuuzi wa Dizaini hii.. kama huna Omba matangazo ya Tigo au Airteli au Lipstiki ya wema ujaze nafasi upate kidogo dogo... KUMUINGILIA RAISI WETU NA WATU WAKE (SISI WATANZANIA- MIMI NA WEWE) NASEMA STOP STOP IT... HAIJENGI HAIJENGI...NA HATUTAKI TENA KABISA UPUUZI HUUUUUU... STOP IT!!!!!

    ReplyDelete
  8. Kama Humjui Magu (JPJM), Pole sana... Magu tumemuamini na Tumempa nchi ili aweze Kutuvusha na Kuiongoza Safari yetu ya Maendeleo.. Kazi ni Ngumu na Amekubali kuchukua hii heshima tuliompa katika wakati Mugumu wa kila sehemu Hewa..Hewa.. Sasa kwa Taarifa yako mwandishi na waliokutuma na wanao kutumia tunakwambieni .. KICHWA CHA HABARI NA MAUDHUI YAKE .. NI choko choko isiyo na Mashiko na Msukumo unaonekana unachembe chembe za Chama na Chuki binafsi... Nisicho kijua kuhusu we mwandishi dhamira yako na Lengo lako?? Kumbuka na Ujue Mtukufu Raisi JPJM na Sisi hatutetereki wala kujibu katika Gazeti wala hapa Uppuzi wako na Usirudie tena kutuwekea Upuuzi wa Dizaini hii.. kama huna Omba matangazo ya Tigo au Airteli au Lipstiki ya wema ujaze nafasi upate kidogo dogo... KUMUINGILIA RAISI WETU NA WATU WAKE (SISI WATANZANIA- MIMI NA WEWE) NASEMA STOP STOP IT... HAIJENGI HAIJENGI...NA HATUTAKI TENA KABISA UPUUZI HUUUUUU... STOP IT!!!!!

    ReplyDelete
  9. Yaani mnajitahidi sana kumwaga sumu,lakini mimi kwangu ni sawa na mbuzi kumpigia gitaa.Hainingii akilini hata kidogo.

    ReplyDelete
  10. Mwandishi shwain zako,kwa nini unapenda kuandika mabaya tu?Hufai katika jamii kwa kuwa sijaona ukisifia mazuri yanayofanywa na muheshimi rais,tena yafaa upunguziwe umri wa kuishi wewe.Ulaaniwe.

    ReplyDelete
  11. Mbona Mhe, Maghufuli hasemi kuwa JUBILLEE wana urafiki na UKAWA? kila mtu na rafiki yake hakuna mtu wa kumchagulia rafiki mwenzake. Pili Mhe, Maghufuli na Odinga ni marafiki toka huko siku za nyuma, ina maana kwa kuwa r maghufuli kapata urais basi avunje urafiki na Raila kwa sababu Raila hasimu yake mkubwa ni Mhe, Uheru Kenyatta?acheni matatizo na mikasa nyie chadema na Ukawa wenu.Tufahamu nyie ndiye source wa Kenya ila itafahamika na aliyehusika ni kuwekwa ndani ili aseme ukweli wa mambo. Nimekuwa nikisema kuwa hao mlio wapokea toka ccm watawaponza walishazoea fitna na wizi na pia ni mafisadi na wezi wa ardhi. Wote mtaaeleweka hivyo na watawarudisha nyuma kisiasa. Kuna chama kinakuja uenda ndicho kitakuwa mbaala wenu kwani wengi wanajieungua kutoka ndani ya ukawa baada ya kuona hakuna VISION.

    ReplyDelete
  12. BEN SAANANE,WA KUJUBU YAYO NI MH.MBOWE NA CHADEMA NA SIO MAGUFULI.
    AU UMESAHAU NINI CHADEMA WALIFANYA?WEE KILAZA?

    ReplyDelete
  13. Umetumwa?
    Ni bora urudi kwa aliyekutuma arudi kwenye kumbukumbu zake aone ni namna gani hayuko makini na taarifa/kazi zake.PUMBA..........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad