Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.


Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi,

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki alipokuwa akifungua Mkutano wa siku mbili  wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.

 

Lengo la mkutano huo ilikuwa ni  kujadili masuala ya Afrika katika kukuza utawala wa sheria katika utekelezaji wa agenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na agenda ya Umoja wa Afrika ya 2063.


“Mkutano huu wa kistoria nchini Tanzania utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi zinazosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za Afrika”, alisema Waziri Kairuki.


Akiendelea kuzungumza Waziri Kairuki alisema uwepo wa Marais wastaafu kama Mhe.Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya Kikwete, katika mkutano huo ni ushahidi tosha wakuwepo na mafanikio ya utawala wa sheria na utawala bora nchini Tanzania.


Kwa upande wa Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa, amesema ili Bara la Afrika liendelee Kiuchumi ni lazima watu wake wapate elimu ya uraia ili waweze kushiriki zaidi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao pamoja na kuwepo na uongozi utakaoleta mabadiliko “transformative leadership”.


Naye, Waziri wa Haki Sudani ya Kusini Mhe. Pwanauwilla Unango amesema pamoja na kuwa Bara la Afrika lina matatizo mengi kama vita, njaa, magonjwa na ndoa za utotoni, dunia isiitazame Afrika kwa mtazamo huo pekee, bali inahitaji msaada kutoka Jumuiya za Kimataifa.


Mkutano huo wenye kauli mbiu “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063:Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, (Achieving the 2030 agenda and agenda 2063:The rule of law as a driver of Africa’s suistainable development) , umeandaliwa na  Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) la nchini Italia, kwa Ushirikiano wa Serikali ya Tanzania  umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu.


Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acheni kuwahadaa watu.angalia Bunge, uchaguzi uliopita.ni nyinyi viongozi vigogo mliopita mmesabBisha mengi.hatuwategemei musema ukeli

    ReplyDelete
  2. Big Five!! Especially the current government..it's governance is second to none..From its core style..it's targets. it's performance IT'S Dedication. it's achievement..what i can say it's a win win situation in all fields.. The Aim is Good the team is responsible and excellent..Mungu akupeni afya na umuri mrefu..tuweze kufikia malengo chini ya JPJM

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi ni nini maana ya utawala wa sheria!!? ni sheria kuelemea upande mmoja au ni sheria inayokata kuwili? basi tunaomba sheria iwe na makali kote kote au vipi?

      Delete
    2. mdau, sheria ni kama panga. usipo ikata ina kukata.. kwa hiyo unaishi kwa Uaminifu na Uadilifu.. itakulinda..upo mgosi??

      Delete
    3. Wee ujamuelewa mwenzio, mwenzio anamaanisha sheria isigemee upande mmja tu. Yaani kwa raia wa kawaida wasio na uongozi wowote bali iwe kote kote balance na kama ni msumeno uwe kote kote. Yaani kwa viongozi watakao haribu maslahi ya nchi na wale wananchi wa kawaida wote sheria iwahukumu, sio imuhumu mwanachi wa kawaida ti. Maanake tumezoea kuwahukumu waiba kuku tu na wale wezi wa mali za umma. Ubadhilifu ufisadi wizi wa kupitiza sheria hawabani hao eti madai viongozi ndio tuibiane, wanatuibia wanachi wa kawaida, mwisho wa siku tunakosa huduma muhimu. Sasa sheria iwekwe iwe inawahusu sanaaa tu, la sivyo hatuwezi endelea, tutazidi itwa nchi za dunia ya tatu mpoo hapo

      Delete
  3. Sasa ifikie wakati, iwekwe sheria kwa hawa viongozi wa juu, atakayeribia Taifa na lujilimbikizia, na kuachia nchi kama inajiendesha yenyewe kwa kuwa hakemei corrupition na yeye raisi ni corrupt, akimaliza muda wake na ashitakiwe na kuhukumiwa kwa ubadhilifu wa uongozi mmbovu na wizi ufisadi uliokirhiri, ndio hiyo midomo yao itawashuka, maanake wamezoea kuongea tu vitendo ni ziro. Hawa wote waliopita, ukiacha Mwl nyerere

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad