Serikali Yatoa Msimamo Wake Kuhusu Mapenzi ya Jinsi Moja ya Mashoga na Wasagaji

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju amesema kuwa mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki na Serikali ilishaweka msimamo wake katika hilo.

Akizungumza mapema leo katika mkutano wa wadau wa haki za binadamu uliofanyika katika hoteli ya Blue Pearl wa kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu (Universal Periodic Review), Mhe. Mpanju ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema  mapendekezo yaliyowasilishwa Mwezi Mei mwaka huu katika mkutano wa Baraza la haki za binadamu uliofanyika Geneva, serikali ilikubali mapendekezo Mia thelathini (130) na mengine 72 iliyakataa.

“Sehemu ya mapendekezo hayo serikali iliyakataa kwa sababu kuna mengine yapo kinyume na katiba, sheria, mila na desturi zetu, kwani katika mapendekezo hayo yapo yanayotaka mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo haliwezi kukubalika”, Mhe. Mpanju alisema

“Hivyo wakati mkijadili namna ya kupanga mikakati ya utekelezaji ili serikali ione umuhimu wa kukubali sehemu ya mapendekezo hayo naomba msijielekeze kwenye yale yaliyo kinyume na imani”, Mhe. Mpanju alisisitiza

Aidha, Mhe. Naibu Katibu huyo alisema serikali imefungua milango kwa kushirikiano na tume, wadau wa haki za binadamu wapeleke serikalini  sababu zenye mantiki ili kuona ni mambo gani  ambayo serikali inaweza  kuyashugulikia na kuyatekeleza.

Akizungumza katika Mkutano huo, Bwana Onesmo Olengurumwa kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) alisema kuwa wadau wamekutana katika mkutano huo   kujadili ni kwa namna gani wataishawishi serikali ili iweze kuyakubali mapendekezo yaliyobakia na kuyaweka katika utekelezaji.

Akifungua mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Iddi Mapuri alisema kuwa mkutano huo umelenga katika kuweka mikakati ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo hayo na alipongeza mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha masuala ya haki za binadamu yanapata msukumo mkubwa hapa nchini.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na Haki za binadamu kwani inakiuka matumizi halisi ambayo Mungu aliyo yaweka kwa binadamu wote wanaodai uhalali wa mapenzi ya jinsia moja serikali itengeneze kifungu cha sheria yenye hukumu ya kifungo cha maisha.Inasikitisha sana kuona mwanaume amechoka kuwa mwanaume anatamani kuwa mwanamke atumiwe na mwanaume mwenzake na mwanamke pia vivyo vivyo huu ni ushetani kabisa kabisa

    ReplyDelete
  2. Kuowa wanawake 10 ni ruhusa
    Fyuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. tanzania acchen uonevu na wanaofina why msiwazuie mana nikinyume piaaa..tena wanafila wake zao na watoto washulee sasa jinsia moja why msiwaache wakapata nao haki zao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad