Shilole Alia Wasanii Wenzake Kumdhalilisha

Msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameonesha masikitiko yake kufuatia madai ya kudhalilishwa na baadhi ya wasanii wenzake kwa kuipa promo video ya wimbo mpya wa zilipendwa wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ wa Jike Shupa.

Kwa mujibu wa Shilole, video ya wimbo huo inaonesha matukio ya kumdhalilisha ambayo inaonekana yeye alikuwa akimfanyia Nuh enzi za uhusiano wao kama vile kumpiga na kumzodoa, mambo ambayo hakuwahi kuyafanya.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya wasanii wenzangu kuiposti video hiyo kwenye mitandao mbalimbali, huko ni kunidhalilisha kwa sababu jamii ikiangalia inaweza kunitafsiri tofauti,” alisema Shilole.

Katika video hiyo, msichana anayefanana na Shilole aitwaye Zuwena aliyetumika kama video queen anaonekana akimfanyia vitimbi Nuh huku akitafsiriwa kuwa, ndivyo Shilole alivyokuwa akimfanyia jamaa huyo.

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hudhalilishwi hivo ndivo ulivyo kuwa binadamu na ujuwe kuwa wewe ni mwanamke na utabaki kuwa mwanamke

    ReplyDelete
  2. kumbe kwa nini tusi msapoti Nuhu Mziwanda nyimbo nzuri sana ugomvi wenu inahusu tusi msapoti kila mtu ana uhuru wake tumependa halafu big up Nuh umetoka kwenye mdodmo wa papa

    ReplyDelete
  3. Shilole kila mara wewe kazi yako ni kutafuta kiki ndiyo maana hatuwezi kukusikiliza kitu chochote unachosema

    ReplyDelete
  4. Achana nao maisha yanaendelea iwe kweli au si kweli bado life itasonga tu jipange upya fanya kazi always kuachwa kuna uma hasa ukiwa hujajipanga,,,kwa mimi binafsi Nuhu alikua hajajipanga ndio maana kaumia sana kupigwa chini,,,wewe sio wakwanza kutukanwa na wala hutokua wa mwisho.

    ReplyDelete
  5. kwa tabia yake shilole ni mchekeshaji hata ajipange vp she will remain to be entertainer huo sio ujabari mwanamke ni mwanamke you should have qualities na sio kuwa mchekeshaji rudi nyuma jiulize je why naambiwa mchekeshaji labda utajirudi lakini kwa umri ulionao sijui........ Nuh he too young tafuta size yako

    ReplyDelete
  6. Jinga kweli wewe.....unajishuku eeeee??!Acha ufundwe maana unapenda dogodogo ili uwanyanyase tu......Ungekutana na dogo janja kama mie kitimbi ungekula wa chuya wewe na uzee wako

    ReplyDelete
  7. halafu usijianike ovyo unakera sana yani unajiumbua mwenyewe huna hata hamna atakae kuonea huruma labda wale hasara hasara kama wewe hupendezo mtoto wa kiislamu kuw hivo mbn unatapatapa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad