TAKURURU Waendelea Kuchunguza Waliopokea Pesa za ESCROW..Mkurugenzi Asema Wasizani Wapo Salama

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema watu waliopokea mgawo wa fedha zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, hawako salama kwani anaendelea kuchunguza nyaraka.

Amesema uchunguzi wa sakata hilo la uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo unahitaji umakini mkubwa, ukikamilika wote watakaobainika watachukuliwa hatua.

 Mawaziri wawili (Profesa Sospeter Muhongo na Profesa Anna Tibaijuka), waliwajibika kutokana na sakata hilo, viongozi wa kamati za Bunge (Andrew Chenge, William Ngeleja na Victor Mwambalaswa) kuvuliwa madaraka, wanasiasa kufikishwa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na watumishi wengine kufikishwa mahakamani.

Chenge na Profesa Tibaijuka waliwajibishwa kutokana na kuonekana wameingiziwa Sh1.6 bilioni kila mmoja kwenye akaunti zao, Ngeleja (Sh40.4 milioni), wakati Mwambalaswa aliwajibika kutokana na mgongano wa kimaslahi.




Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Porojo nyingi sana hii nchi sasa kwanini usikae kimya ukaja na matokeo? Uchunguzi Wa miaka mingapi wakati report ya zitto iliwataja na mpo nao bungeni wizarani majirani zenu na ni marafiki zenu? Jamani mtuonee huruma watanzania sio kutuona wajinga sisi sio wajinga ni wavumilivu tu. Haina haja ya kuita waandishi na kutoa porojo kaeni kimya kuleni hizo hela maana si mmeona ni zenu peke yenu? Ila mjue kuna mungu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad