Tanzania Kutengeza ndege Aina ya Helikopta...

Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linatengeza ndege .Gazeti la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi .

Gazeti la Zambia,Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.

Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hili ni Jambo zuri. Hizi ni prototype of helicopter. provided TCAA wameziidhinisha baada ya kuangalia na kuridhishwa na safety features na evacuation na usalama wake katika anga zetu hii itapelekea utashi wa kutaka vijana waweze kujifundisha pilotting na kuweza kuwa launching pad wa kutaka maendeleo zaidi ya kufanya mengine na kujifundisha zaidi. Aviation is a vast economical engine drive na mwanzo ndiyo kama hivi na inaweza kuwarubuni wawekezaji baada ya kuona kwamba Tanzania ni nchi ambayo inawezekana kufanya biashara na kukaribisha mataifa kama Brazil na shirika la Bell la Canada na wengine wenye uzoefu wa kutengeneza hizi helicopter. Na Wachina waweze kewekeza katika utengenezaji wa Magari hapo tutaweza kujenga Ajira na transfer of technology... Pole pole lakini ndiyo tuko njiani... Tutafika inataka Subira na ustahamilivu huku tukijipanga na strategies with a Vision... hongera sana baba JPJM na mwelekeo huu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad