TCRA na uzimaji wa simu: Ni sanaa, propaganda, utani au ufinyu wa teknolojia?

Kwa Karibu mwezi mzima kumekuwa na Habari ya Kitaifa kuhusu Kuzimwa kwa simu feki.

Tukapewa na namna ya kuzitambua hizo simu feki kupitia mfumo wa namba za IMEI (International Mobile Station Equipment Identity).

Huu utaratibu ulikuwa unatambua IMEI ambazo ni "null" yaani hazipo kabisa na nyingine ambazo ni "duplicates" yaani zinashabihiana na simu nyingine ambayo ni halali. Tukaambiwa kutakuwa na uzimaji wa hizo kupitia mtambo au mfumo maalum na wa kisasa kuzinyima fursa ya kupata mtandao (Network Access).

Lakini kinachotokea baada ya muda huo kufika ni simu nyingi kuendelea kuwa hewani mojawapo nimeshuhudia mimi ambayo ina IMEI ya "duplicate" na jina la Darago lakini simu inaonekana ni "Nokia" zikiwa na model tofauti ,na kadhalika kutoka kwa watu wengine ambao walithibitisha kuwa simu zao zitazimwa.

Maswali yangu kadhaa ili kujua hili zoezi ni Sanaa,Propaganda, utani au Ufinyu wa Teknolojia mahususi ni kama ifuatavyo:-

1.Je Elimu haikutolewa vyema kiasi ambacho simu tulizojua zinazimwa hazikuzimwa?

2.Je Teknolojia ya mfumo wa kuzimia ina mapungufu ambayo yameufanya kushindwa kuzizima hizo simu?

3.Zoezi la uzimaji simu:TCRA hawakujiandaa au kufanya majaribio kabla ya kuchukua hatua?

4.Je hakuna siasa katika suala zima linaloendelea kuhusu uzimaji wa simu "Standardization" ?

5.Nini hatima ya wale ambao hawajazimiwa,Je simu zao ni halali kisheria au waendelee kukaa na wasiwasi? (Hapa naweka angalizo Isije kukawa na kesi nyingi za kuflash simu)

6.Maswali mengine Ongeza wewe!!!!!

---------------------------
Nesto E Monduli
Chanika,Dsm
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi kwaakili yako ww mleta mada na watanzania kwa ujumla mnazani kuna mtambo mtambo wa kuzima sm feki dunuiani? Km wangesema tunazima network ya Tigo, Vodacom, Zantel nk. Hapo ni sawa lkn sm uko nayo ww kwako halafu aizime mtu aliye nje ya nyumba? Sm feki zipo mpaka nchi za watu wenye akili na watu wanabofya kana kanaida

    ReplyDelete
  2. Hakuna sanaa hapo hata Mimi nimeshuhudia kwa macho yangu Kuna simu zimezimwa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad