Tulia Akson Aendelea Kususiwa Bunge na Wabunge wa Upinzani..Hichi ndo Kilichotokea leo


Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena  wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.


Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje  majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.


Kambi  upinzani  ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale "haki itakapopatikana."


Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya majina ya KIONGOZI WA KAMBI RASMI ?? Yana maanisha nini ubenge wa Hai au? kinachodaiwa ni ukandamizwaji wa Demoklasia? haya pia aliyesimamishwa anayasema hivo pia! Mama Tulia ameweza kuwadhibiti wao wapeita " VITISHO NA UOGA" Hivi namuulisha huyu lingi leader wao... haya matamshi anafundishwa na nani na kwa mwelekeo gani.. Je haoni kuwa yamekusa dhana ya Uzalendo na yamejaa chuki za kibinafsi...

    ReplyDelete
  2. Bomu la Migiro
    Tunataka katiba mpya
    Spika,naibu spika na waziri wa sheria wasiwe wabunge wa kuteuliwa na rais

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna akili wewe hujui hata ni kitu gani unachozungumzia. Unafikiria kwa kutoteuliwa na Rais kutaondoa ukweli kuwa Wabunge wakifanya makosa ya kukiuka sheria na kanuni za bunge hawataadhibiwa. Sheria zitabakia pale pale na pengine zitakuwa kali zaidi ili kuwadhibiti hao Wabunge feki ambao hawana hoja zozote za maana zaidi ya kutuletea uhuni na maupuuzi yao pale mjengoni.

      Delete
  3. watatoka sana na bosho pia wasusie na tulia ndo ataogoza bunge mpk liishe kwani kutoka nje ni sulihisho?

    ReplyDelete
  4. hwana akili hawa jamaa pamoja na majina wanayopeana hayana kichwa wala miguuu eti kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani, wakibanwa wakiona hawana pakupumulia wanasema eti hatuna imani na tulia kumbe tatizo liko kwako wajinga hawa tumewapeleka bungeni kuchota hela tu na wanatafuta namna ya kujipumzisha si waseme tu wwatike wasitoke bunge litaendelea imani na tuli ni mkeo?

    ReplyDelete
  5. Tatizo hapo ni kasi ya Magufuli. Wataisoma namba mwaka huu HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  6. Mbowe tafadhali tumis neno Mimi na wala usitumie Sisi..wewe waliokuleta hapo ni watu wa Hai..na wakiona vioja vyako watachukua uamuzi stahiki juu yako...HAPA KAZI TU..Wajibika na usianzishe ugawanishaji wa makundi..we ni mmoja wa ma mia ya wabunge jua Huzidishi wala hupunguzi ukiwepo au usiwepo..shughuli za Bunge letu tukufu zitaendelea kama kawaida zilivyo pangwa..kama unaahisia kwamba umechoka na unahitaji lokizo wewe omba tu..kumbuka posho itakatwa kila usipo hudhuria labda ukiwa uko hospitali kiafya...Je Una matatizo ya Afya????!!!

    ReplyDelete
  7. tena mboe angalia sana usije ukawa chambo wenzako wanakuitikia tu lakini mchjana mbowe usiku tulia kuwa makini na maamuzi unayoyasimamia yapime kikamilifi kama wote ni njia moja ya kuwapeleka jehanamu au mnataka kwenda peponi lanini naona kabisa mboe utaumbuka mbeleni watakuacha ukienda jehanamu peke yako wapizani wanafiki tuliona mfanop dhahihili pale mlipotuambie lowasa ni fisadi namba moja tanzania lakini mkatukeuka mkarudia kul;a matapishi yenu na kumuingiza katika ukawa tena kwa kuihujumu demokrasia na mkampandisha cheo na kuwa mgombea uraisi mkavunja katiba zenu leo hii mnasema tulia amevunja kati tangulieni kurekebisha kwanza makosa yenu mlioyafanya wakati wa mchakato wa uchaguzi ndio mtuambie habari hizo kiukweli bado hamjitambui mkiweka wazi juu mchakato ulifanyika ili kumpata mgombvea wenu edo ndipo tutakapojua kweli nyie mnauchungu na wananch vinginevy ninyi wote waongo tena mmeacha mpaka leo wanachama wenu wengine wanamaumivu jinsi milivyo fanya kipindi cha uchaguzi kwendeni zenu msihudhuri lakini bunge mwendo mdundo litaendelea tumieni akili, kweli nimeamini sio kila akili inakaa kichwani akili nyingine zinakaa mgongoni mbowe kiukweli tumewachoka sana tena mnajitahidi kumpunguza kasi maguifuli lakini tumewagundua poleni sana lile tingatinga bwana sio kiivyo mbowe simama mwenyewe

    ReplyDelete
  8. kasi ya magufuli inawatesa sana mnaamua kutafuta visingizio Tulia uko sawa mama piga kazi na msimamo huo mama

    ReplyDelete
  9. badhi ya wapinzani nikiwaona nasikia kichefuchefu, mpaka kutapika

    ReplyDelete
  10. pole mboe unatafuta kiki unafikiri rais anatishika na wewe tunamuombea watanzania

    ReplyDelete
  11. tumesema sana humu kuwa hiki ndio kifo cha upinzani na hayo waliyotaka yaweyanaonyeshwa live kwa wananchi wao.
    Kitakachofuata ni matamko ya wananchi walio wachagua mizigo hii kusema HATUNA IMANI NA HAWA tuliowachagua JE TURUDIE UCHAGUZI??? Maana majimbo yenu yanakosa uwakilishi,,twendeni tuone kama mtarudi mjengoni!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad