Tunafanyaje Hili la Naibu Spika Tulia Ackson Kukataliwa na Upinzani?

Ndugu zangu,
Swali hili lilipaswa wajiulize Wabunge wa upinzani wenye kutoka Bungeni kila baada ya dua ya asubuhi.

Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.
Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi Bungeni.

Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura.
Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni kukosekana kwa umakini.

Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale.

Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang'atuke kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu zetu kimfumo.

Yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au Mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.
Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda Serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.

Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.
Maggid Mjengwa,

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu nisamehe huyu mama simpendi jamni yani huwa namuona sijui vipi...nisiongee sana nisije nikafungwa bure

    ReplyDelete
    Replies
    1. anakula kwako???????

      Delete
    2. KWA NINI UMCHUKIE BINADAMU MWENZIO?KAKUFANYAJE?WEE NADHANI UTAFUNGWA NA MUNGU KAMA HUTATUBU.

      Delete
  2. Mjemgwa gombea na wewe ubunge
    Utajuwa ya bungeni
    Wapinzani si wajinga kwani hawapewi nafasi ya kusema maoni juu ya serikali
    Hata hotuba zao lazima zikwatwe
    Sasa kuna umuhimu gani bora watoke wanainchi tujuwe kilichopitishwa ni cha ccm na wabunge wake

    ReplyDelete
  3. Maggid, ulichisema inataka mtu mwenye Akili Na upeo nzuri akichangua budasa ndani yake.Hawa tunao waits waheshimiwa ..imedhihirisha kuwa bado hawajafikia kiwango ambacho wanategemewa..uchambuzi wako Na nasiha zao Ni nzuri..hapa kazi tu

    ReplyDelete
  4. Kwasisi tunaojua siasa, tuliobobea katika Siasa, katika hili la kutoka nje ovyo ovyo kisa wanamchukia mtu na kuanza kupingana na Utawala wa Sheria ili watupeleke katika Uatawala wa Mazoea; UKAWA wameuvaa mkenge; CCM wamefanikiwa kwa asilimia miamoja (100%). Busara, Uwezo na Akili kubwa ya kutambua mambo ya Dr. Slaa sasa inaonekana dhahiri shahiri kukosekana ndani wapinzani.Wamekosa mtu mwenye uwezo, wamebaki na watu wa mob Psychology, ndo maana wanaamini katika Maandamano na Mikutano.WAMEGOTA.

    MTANZANIA

    ReplyDelete
  5. I DONT LOVE THIS WOMEN HAJIELEWI YUPO KWA KUEKWA

    ReplyDelete
  6. Kama kwetu vijiji watakuuliza sawa umetetea demokrasia je imetuletea maji, au barabara inapitika. Wananchotaka wao zile changamoto zinazowakabili zitatuliwe kwanza ndo mengineyo Yafate. Wapinzani waliangalie Hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad