UDART Wazindua Kadi ya Mabasi Yaendayo Haraka

Kampuni ya UdaRT imeanzisha mfumo mpya wa kadi za kielekroniki kwa ajili ya malipo ya nauli kwa watumiaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka.

Mkurugenzi mtendaji wa UdaRT, David Mgwassa amesema kadi hizo zitaanza kuuzwa kesho katika vituo vikuu vya mabasi vya Kimara, Ubungo, Morocco, Gerezani na Kivukoni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Afrika ambao ndiyo watengenezaji wa kadi hizo, Juma Rajab amesema bei ya kadi hiyo ni Sh 5,000 na itakuwa na Sh 4,500 ndani yake ambazo abiria anaweza kuzitumia kama nauli kwa safari nane.

Ameaema kadi hizo hazitakuwa na namba ya siri na kuwa kiwango cha juu kitakachowekwa katika kadi hiyo ni Sh30,000.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad