UKAWA Kususia Futari za Viongozi wakuu Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Dhihaka kwa Waislam

Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa wasiojua ni nguzo mojawapo kubwa katika Nguzo kuu za dini ya waislam. Na mwezi huu kwa waislam ni mwezi wa kufututrishana kusamehehana na kuombeana mema. Ata kama mnaugomvi mkubwa wengi huwa wanausubiri kwa ajili ya kusameheana ni mwezi wa rehema kwa waislam, Lakini kwa nchi yetu hatujafikia hatua mbaya ya kususia ata chakula au maji .

Ukawa wanachofanya ni kutaka kutengeneza Chuki baina ya watanzania ifikie hatua hatuzikani kisa siasa, Najiuliza tu km kiongozi wanayeshindana nae hakifiwa na mtu wa karibu yake Je wapo tayari kumsaidia au kumfariji??

Kama wameweza kususia Futari kisa yupo Naibu Spika?
Watanzania je tumefikia hapo?
Tags

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HEEE KAZI KWELI KWELI SIONI SABABU YA WAO KUSUSIA FUTARI KAMA NI KWELI!!!!

    ReplyDelete
  2. Kadri siku ziendapo Mwenyezi Mungu anatubainishia maadui wetu watanzania hawa UKAWA hawatufai hawatufai watatufikisha kubaya siasa na demokrasi imekuwa ni shida wanaitumia kuganga njaa zao hawana lolote la maana na wako tayari kutuona hata kuzikana hatuzikani sababu ya siasa zao uchwara na watashangilia jambo ovu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Namjue UKAWA si jina tu bali ni mkusanyiko wa watu wengi wenye utashi na fikira tofauti ambao wanajitambu sana, sasa endelezeni huo ubabe wenu wa kuwanyanyasa mwisho wa siku mtaunda chuki na simanzi kwenye hao watu ambao ni wengi na nyinyi mnalijua hilo! Mmekazana ukawa ukawa utadhani ni mkusanyiko wa wanyama kumbe binadamu!! Poleni sana ccm ambao mmeamua humu kuwashambulia Ukawa kwa nguvu zote mkizani mtawaconvince watu wamuone ukawa (mnyama) ni mbaya!!! REMBERE PEOPLES IS POWERRRRRR

      Delete
    2. nyambafu wewe anony 6.32pm sasa hapo umeandika nini?

      Delete
  3. Hakika inashangaza sana,na hii ni kukosa hofu ya Mungu, na yote hayo yanaletwa na Mbowe.Pengine kwa kuwa Mbowe sio muislam na kwamba hafungi basi kwa suala la ftari angewaacha walio waislam waendelee kushiriki na kufuturu,sio na si vyema kumzuia muislam akatae mwaliko wa futuru.maskini wengine hawapendi bali wanaburuzwa kwa kuogopa kuonekana ni wasaliti.Wako watu walioshangaa kuona JPJM alipoenda muhimbili kumjulia hali Mh.Sumaye,wako watu walioshangaa kuona anaenda kumuona Maalimu Seif pale hotelini, jamani tusifikie huko.TZ bado tunaishangaza dunia kwa mambo mengi.Ni ngumu kwa nchi nyingine kumkuta kiongozi wa dini ya kikristo na shehe wako pamoja wanajadili mambo ya taifa,lakini TZ iko hivyo,wanajadili amani,wanaongelea namna gani wawafundishe watoto wao masuala ya imani bila kuwapotosha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Big up mdau,Mimi sio mtanzania,ni wa comoro ila nimeishi sana tanzania,lakini uliosema naunga mkono,angalia hata nchi zinazowazunguka ni ipi inafanya kama tz?Munasema nyie maskini,hicho bado ni kilio kikubwa kwa nchi zetu za afrika,na hio ya miaka 50 ya uhuru bado watoto wanasomea chini,nimetoka india na nimeona kuna maeneo watoto wanasomea chini bado,maji shida,lakini wana amani na kuamini kuna siku hali itaisha.Ombeeni sana amani mlio nayo.

      Delete
    2. shuguli ya kislam shehe ndo mkuu wa shughuli

      Delete
    3. Wewe ni mnafiki sana asee, juzi kati JPM kafuturisha, tumeona hao unaosema waislam walivyopaka mbovu kwamba iweje yeye mkristo afutulishe waislam, ya kwamba hicho ni chakula kama chakula cha dinner!! leo oh!! ni nguzo kuu!! ebu acha unafiki kafuturu nyumbani kwako...

      Delete
  4. Futari hiyo imendaliwa kisiasa
    Na wao na matatizo
    Kisiasa
    Ukawa si wajinga
    Kama msiba watakwenda hata uwe kwa naibu spika
    Acheni longa longa hapa
    Ukawa bingo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si bure wewe,Huna dini na tena mchochezi mkubwa,ULAANIWE!

      Delete
    2. Laana unayo wewe kafiri
      Moto wa kiama na akhera unakusubiri

      Delete
    3. Laana unayo wewe kafiri mkubwa
      Tangu lini futari ikawa na mgeni rasmi zaidi ya shehe

      Delete
  5. Futari allike waziri mkuu
    Mgeni rasmi naibu spika
    Hatujaona haya tangu zianze hizo futarisha
    Hata Enzi ya pinda alipofutarisha
    Makinda hakuwa mgeni rasmi
    Waislam hivi kwenye futari kuna mgeni rasmi au mwandalizi wa futari ndo mkuu wa shughuli nzima
    Naona hapa kuna kulikoni
    Hii si futari
    Tunatumia vibaya kufututisha
    Na kuandaa karamu
    Ukawa hongera sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kuwa akili yako umeshaiweka kwa
      UKAWA basi hata ukisikia wanafanya jambo baya huwezi kupinga?Alichokifanya Pinda sio lazima na Majaliwa aige kwani ni sheria au ni lazima kufuturisha?
      Mlipinga sana wakati serikali inapinga chama pinzani kuwa na walinzi wao,na kujaribu kupambana na wale wote waliokuwa wakijipanga kwa hilo,sasa kwa hilo kwa nini tusiamini hata hao vijana wadogo wanaokutwa wanafundishwa ugaidi wametokana na vyama pinzani?Sina chama na wala sikupiga kura kwa kuwa sikuwa Tanzania wakati huo,lakini ninachoweza kusema JPJM apewe ushirikiano,kwa kuwa hata yeye mwenyewe anasema ni rais wa wote,na ni kweli.Mungu ibariki TZ.

      Delete
    2. Koma wewe magaidi hawana chama wala dini wapo kila kona fyuuuuu
      Wapo ccm wapo ukawa wapo kila kona
      Akili finyu
      Mmezoea vya dezo
      Na kuvaa sare na kanzu
      Kumbe wanafiki

      Delete
  6. KAZI KWEKWELI UBAGUZI NI DHAMBI SAWA NA KULA NYAMA YA MTU

    ReplyDelete
  7. KAENI CHONJO NA HAO UKAWA

    ReplyDelete
  8. TUMEKATAZWA NA MUNGU KUCHUKIANA. JE? WAO UKAWA MUNGU WAO NI YUPI?

    ReplyDelete
  9. Futari nayo inakuwa na mgeni rasmi!!!!! alafu wewe unayasema Mbowe hafungi una uhakika gani? kwa sababu sisi wakristo tukifunga hatutangazi Biblia imetukataza kufanya hivyo, na pia sio lazima ukimwalika mtu kuja kula lazima aje. Mtu ana uamuzi wa kuja kula au kuacha hiyo ni hiari ya mtu. Usilete uchonganishi hapa. Eti akifiwa hawataenda!!! lo kwa hiyo unalinganisha msiba na futari (chakula)?

    ReplyDelete
  10. Futari futari futari, naona kama ........

    ReplyDelete
  11. Yani mm naongelea kwa upande wangu mm kama sikupendi ni bora nikae mbali na ww yani mbali kabisaa si futari si mwezi utakaotuweka pamoja ndo nipo hivyo Mungu na anisamehe huo ndo udhaifu wangu kuwa karibu na mtu anayenikwaza nikijifanya nafurahi uwepo wake nooop kwangu mm hiyo hamna hakuna unafki yani tukae mbali tu nadhan ndo majeraha yangu yatapona haraka na kwa kuangalia hapa ni kama kuna kukomoana flan hv...so waachen tu ukawa...mm bora nisifunge maana kama nakuchukia nitakuwa najitesa na njaa tu sijui kusamehe haraka M/Mungu nisadie...unafki wa kukaa pamoja kisa mwezi mtukufu halafu mwezi ukiisha uadui unarudi palepale...khaa na mnayaweza

    ReplyDelete
  12. Ahhhhhh.. Nimesikitishwa na hiki kitendo... Tena sijakitegemea Kwetu hapa TANZANIA.

    Kwa sisi Watanzania na jinsi tulivyo lelewa na kulea watoto zetu. Tofauti ya Dini haina gap kubwa baina yetu .. tumecheza pamoja/ tumesoma pamoja/ tumekwenda jeshini pamoja/ tumefanya kazi za ujenzi wa taifa pamoja.. tumeweza kungojeana kwa baada ya ibada zetu ndiyo tuanze safari yetu kama ni za matembezi au kutembelea wagonjwa mahospitali.. Na hii tumedumunazo katika maisha yetu na tumeweza kuheshimu dini na ibada zetu ipasavyo.

    Mwezimtukufu wa Ramadhani ni Moja ya nguzo ya dini yetu ya Kiisalamu ambayo tunafundishwa toka utotoni na inatujenga kuwa wavumilivu na wastahamilivu na kuweza kujiweka na kumjua aliye na halii duni zaidi maisha upande wake yakoje..Na mwezi wa ukarimu na karam... mwezi wa kusameheana na kuoba maghfrira kwa mola wetu na kuzidisha ibada na kuweza kuwa karibu na familia na Jamii na watu wako wa mji wako na mikoa yanu na Taifa lenu na ulimwengu kwa ujumla..Leo nikikwambieni hapa Obama anaalika wana Diplomasia wote Wa nchi za Kiislamu na wasiokuwa hii ni kwaajili ya Nini? inathibitisha kuwa Tunaheshimu na kuelewa Ramadhani ni Nini halafu pia inaashiria kuwa Dini zetu hazitutenganishi sisi wote ni wamoja na isitoshe inajenga Imani katika maelewano baina ya watu.. Hivi siku chache zilizo pita nilikuwa Malaysia.. Nilipendezewa sana baada ya sisi kualikwa baadhi ya walioalikwa walikuwa ni waMalay wenye asili za Kichina na Kitamil na waarabu niliuliza jee hawa wote wanafunga? Jibu lilikuwa Zuri sana na nikafurahi.. Sisi hapa Malay/Mchina? Muhindi/ Mwarabu / wote ni wamoja na kila mwanajamii wetu katika wakati kama huu anamsapport mwenzake bila kuonesha kasoro..Akaanza kunieleza Historia ya nchi yao baada ya kushikwa na Dr Mahathir Mohammed to katika ukulima wa Rubber tree /Minazi na Mawese mpaka leo Malaysia ni Moja ya Economical Giants of South East Asia.. Nilimuuliza vipi iliwezekana na kwa muda gani... Na kilicho endelea nilisikiliza na huku siamini naamini .. Ilichukua miaka karibu @0 na kidogo.. yote ilikuwa ni kwamba watu walibadilisha Working Culture wakawa wote wameondoa Tofauti zao za vyama .. na aliitwa Dikteta kwa ajili wa wavivu wasiotaka maendeleo na wapenda kusema na alikandamiza panapo hitaji kukandamiza ili alete maendeleo ya jamii na watua baada ya kuona mambo yanakwenda viwanda vinafanya kazi ajira inapatikana .. WAkaondoa tofauti zao na kuanza kujituma zaidi na kina mama wakaaza kukatiwa barabara za toll kwa kilometa na ajira ikawa kila mwanafamilia anawajibika nchi ikawa haina tena gumzo ni kila mtu kazi kwa shifts kila nyanja.. mkulima wa Rubber tree ameondolewa tax na anafatwa huko huko shamba kwa huduma zote shule/hosp/benki/huduma zote sa rekikali na wana serikali yao ya kitongoji kuwathibiti vijana viongozi wa kesho kama iliyofanywa hapo Siha (Kilimanjaro) na Kasalazi (Sengerema) ili kuwaweka katika Maadili hata watakapo fikia wakati wa kuwa watendaji ni kwamba wameshapata Malezi bora na imani bora ya dini zao bila tofauti na ni Taifa Moja na Mwelekeo Mmoja... Na Mpaka sasa Haya ndiyo Maisha yanayo endelea... Hili wa Watanzania Kususiana Futari na Kudhalilisha IMANI kwa kuonesha Kuto Heshimu Mwaliko wa kuadhimisha Moja ya Nguzo ya Dini Yetu ya Kiislamu Hapo Nasema HILI SIYO SAWA NA HALIKUTEGEMEWA KUINGIZWA KISIASA NA SIYO SIASA .. Bila kumtaja jina mmoja wa Waziri wa Awamu ya Nne ambaye tulikuwa Marafiki to kato utotoni... Alikuwa Dini Nyingine na Mimi ni Muislam.. Ilikuwa yeye ananikumbusha wakati wa Sala na tunatoka pamoja kwenda msikitini na ananingoja mpaka namaliza kusali nalafu tunaendelea na mengine hii imejenga Undugu baina yetu na watoto zetu na familia zetu. Na Tofauti baina yetu hakuna ni tumekuwa ndugu hata Vijana wake wamekuja kusoma Na tumeishi nao bila kuona tofauti kuwa mie si mzazi wake.. Anaona ni mzazi na akimaliza anarudi kujenga Taifa.. Naomba toufauti zetu Tusizilete katika HAYA... TANZANIA NI UPENDO / AMANI/ UMAOJA NA USHIRIKIANO WA MILELE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad