UKAWA Wamjibu Naibu Spika.....Wamwambia Posho Akawatishie Watoto

Siku mbili baada ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson kuagiza wabunge wa upinzani wanaoingia Bungeni na kisha kuondoka wakisusa vikao wasilipwe posho, wabunge hao wamejibu wakiubeza na kuupinga uamuzi huo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wabunge wa upinzani wamekosoa uamuzi huo wakieleza kuwa Dk. Tulia alihukumu kesi inayomhusu, kitendo walichosema sio haki.

Aidha, wabunge hao walieleza kuwa posho haitakuwa sababu ya kuwarudisha nyuma kwenye uamuzi wao kwakuwa sio hoja wanayoipigania. Walisisitiza kuwa wataendelea kutoshiriki vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk. Tulia kama walivyoazimia.

“Ukawa haiwezi kutishiwa posho tunapokuwa na hoja na mawazo ya msingi. Hoja yetu hapa si posho, kuna mambo ambayo anayafanya Naibu Spika hayaendi sawa na sio ya kawaida. Hoja ya posho akawatishie watoto, sisi ni watu wazima. Tumekuja hapa tuna utashi mkubwa,” alisema Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema).

Naye Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika unawadhalilisha wabunge kwa kuonesha kuwa posho ndio kitu walichokifuata Bungeni hapo.

“Mimi nimekuwa kwenye siasa kwa miaka zaidi ya 25 sasa. Kilichofanywa na Naibu Spika ni kudhalilisha wabunge, ionekane sasa tupo hapa kwa ajili ya kulipwa posho. Tupo hapa kwa ajili ya kutoa huduma kwa Watanzania. Kina Tulia wakiwa shule ya msingi, sisi tunapambana bila kulipwa posho na mtu yoyote,” alisema Mbatia.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alitoa msimamo wa kambi hiyo kuwa hawatashiriki vikao vyote vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika kwakuwa amekuwa wakiwakandamiza na kupendelea upande mmoja. Pia, Mbowe alisema kuwa Dk. Tulia anaongoza Bunge kwa ubabe akilinda maslahi ya Serikali.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mlio kosa Uzalendo na Kujifanya mna msimamo dhidi ya Bunge la Taifa ambalo nyinyi mnadhaniwa kuwa wamoja wa Active participants.

    Sasa ndiyo iweje???? mmeshachoka na unapoteza mwelekeo!! Posho Inakatwa Hatutaki Kuibiwa na kuchakachuliwa Maana yake mlisha zowea.. sasa muwajibike na Nyinyi kina ndumila kuwili sasa Wajibikeni... Unachezea Posho wewe!!!! wengi mtasema maanake zimewagusa sana na mtesema sana!! Hapa Kazi Tu...

    ReplyDelete
  2. Mlio kosa Uzalendo na Kujifanya mna msimamo dhidi ya Bunge la Taifa ambalo nyinyi mnadhaniwa kuwa wamoja wa Active participants.

    Sasa ndiyo iweje???? mmeshachoka na unapoteza mwelekeo!! Posho Inakatwa Hatutaki Kuibiwa na kuchakachuliwa Maana yake mlisha zowea.. sasa muwajibike na Nyinyi kina ndumila kuwili sasa Wajibikeni... Unachezea Posho wewe!!!! wengi mtasema maanake zimewagusa sana na mtesema sana!! Hapa Kazi Tu...

    ReplyDelete
  3. Poa makamandaaaa posho siyo issue.... tusonge mbele kwa mpamabano ya kudai haki

    ReplyDelete
  4. Issue Ni laivu not laivu

    ReplyDelete
  5. Hawa Ni wazembe Na wavivu..walifikiri wataendelea kuvuta poosho kiulaini...TUMELIKATAA HILO NA HATURIDHIKI NALO ..mpo wahesabiwa....issue sasa Ni nini Kama Ni posho hakuna kila ukitoroka kazini....HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  6. Naibu spika kaza buti walizoea kuchezea akili Za watu wamekutana na anaejua sheria wapi tunda lissu

    ReplyDelete
  7. Watumbuliwe wote ni majipu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad