Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga jijini Dar es Salaam leo.
UONGOZI wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) umekanusha tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Juni 10, mwaka huu katika kijiji cha Nyakabale Mkoani Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga amesema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.
"Mbunge huyo alisikika katika mkutano wa hadhara kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) huwalazimisha wanawake wanaoingia mgodini bila kibali kufanya mapenzi na Mbwa watumikao kulinda eneo la Ngodi"
Tenga amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa uzito mkubwa dhidi ya Mbunge huyo kwani taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kuchafua na kutuharibia sifa mbele ya serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na jamii kwa ujumla.
Amesema kuwa Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) amekuwa akitoa kauli mbalimbali kuwa ni za kichochezi na zinapelekea uvunjifu wa amani kwa wakazi wa Mkoani Geita.
Pia ameviomba vyombo husika vilivyopewaa maagizo kuchunguza tuhuma hizo vifanye kazi yake kwa kuzingatia haki na sheria ili ukweliujulikane na sheria ichukue mkondo wake amesema Tenga.
Uongozi wa Geita Gold Mine Wakanusha Tuhuma za Wanawake Kulazimishwa Kufanya Mapenzi na Mbwa zilizotolewa na Mbunge
2
June 13, 2016
Tags
Wabunge wa ccm hao
ReplyDeleteAu kakosa mshimko
Au ndo majipu ya ccm
Jmanai ukiwa mbunge usiseme jambo bila kijiridhisha ni aibu. Kufanya hivyo mnakiua chama kwa mikono yenu jiangalieni na kujionya ili kulinda hadhi ya chama. Kufanya kosa siyo kosa ila kurudia kosa.
ReplyDelete