Upepo wa Edward Lowassa Wazidi Kuyumbisha CCM

Wabunge wa CCM wameunda kamati maalumu ya wabunge 15 kwenda kutathmini uchaguzi mkuu, badala ya kutegemea ripoti zinazotolewa na makatibu wa wilaya na mikoa pekee.

Katibu wa wabunge hao, Jason Rweikiza alisema kamati ya wabunge hao itawahoji wabunge wote wa CCM 267 kwa sababu ndiyo wahusika wakuu, kuangalia changamoto walizokutana nazo.

Miongoni mwa wajumbe hao ni Joseph Mhagama, Dk Faustine Ndugulile, Joseph Kakunda, Profesa Anna Tibaijuka, Mboni Mhita, Peter Serukamba, Innocent Bashugwa, George Mkuchika, Munira Mustapha, Jasmini Tiisekwa na Abdallah Ulega.

 Katika hatua nyingine, CCM Mkoa wa Ruvuma imewatimua wanachama 62 kwa usaliti ikiwamo kumuunga mkono Edward Lowassa katika Uchaguzi Mkuu 2015.


Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lowasa hufai bwana hebu angalia afya yako ukisema unahema ukisimama unatetema ukikohoa siunajua tena siasa waachie wenye afya zao hapa kazi tu umesahau ulivikuwa ccm au nikukumbushe usituvuruge ccm dam dam

    ReplyDelete
  2. Edward Ngoyai Lowassa... Good Moning!! nasikia pia fedeliki anakuja.. Je kweli? Poleni .. kumbekeni Afya zenu ni muhimu kuliko chochote katika maisha yenu yaliyobaki... Madalaka na kiti nyote vinakuwa havina mpango ikiwa afya imedolola... Mwangalieni Fidel Castro.. Ramol kashika yeye hajui kinacho endelea au kinacho kuja... Furahia maisha yenu yaliyobaki... Utumbo wa siasa na madalaka nakuhakikishieni tuna Kiongozi Jasiri na Muweza na Mzalendo... Hapa ni kazi Tu.. JPJM kashika hatamu na anaweza na anafanya kweli!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad