Shamra shamra zilizolipamba taifa kwa wiki kadhaa sasa juu ya uzimaji wa simu feki hazina tofauti na zile za kuukaribisha mwaka mpya. Huki vijineno na vijimifano vya kiutani vikitembea kwenye social medias, zoezi hili limeonekana kuleta hamasa ya pekeee na kuliunganisha taifa. Watu wa familia wamekua wakipigiana simu kutaniana na kukumbushana kuchukua taadhari juu ya kuzimwa simu, vijimisemo kama vile, 'Hii kazi wangepewa TANESCO ingekuwa imekwisha kitambo, na vijimisemo kama 'ukiona sipatikani ujue niko nje ya nchi', ni baadhi tu ya vikorombwezo ambavyo vimekuwa vikiendelea kwenye social media.
Kiuhalisia ingawa inaonekana ni asilimia chache ya wananchi watakao athirika na zoezi hili, woga flani uemwashika watu wengi wakihofia kupotea hewani, jambo ambalo linaonesha jinsi mawasiliano kwa njia ya simu yalivyokuwa muhimu kwa taifa la sasa.
Wakati tunangojea zoezi hili kukamilika, nawatakia shamra shamra njema.