Uwanja wa Taifa Wafurika...Milango Yafungwa Saa Tano Baada ya Watu Kujaa...

TFF imeeleza kuwa milango ya uwanja huo ilifungwa  saa tano asubuhi kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo na kuingia moja kwa moja uwanjani.

Hadi kufikia saa 11:53 asubuhi, mashabiki waliokuwa nje ya uwanja hawakuruhusiwa kuingia ndani kufuatia majukwaa kufurika mashabiki, nafasi ya kuingia uwanjani imebaki kwa watu maalumu na Wanahabari pekee ambao wanaingilia mlango mkubwa wa Uwanja wa Taifa wakati ile mingine ikiwa imefungwa.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema walilazimika kufungua milango ya uwanjani mapema tofauti na walivyoeleza awali kutokana na mashabiki kufurika uwanjani kuanzia saa tatu asubuhi.
"Mashabiki walianza kumiminika uwanjani kuanzia saa tatu, hatukuwa na namna zaidi ya kufungua milango ya uwanja muda huo ili kuwapa fursa ya kuingia na kupunguza msongamano," alisema Lucas.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tv live bungeni watu hawatofanya kazi saa kazi
    Haya Leo kulikoni tangu saa mbili asubuhi uwanja nasikia saa ushaa jaa
    Mchezo jioni

    Tumbueni na huku au Leo sikuku ?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad