Video Queen Tunda Akwaa Aibu Kali...Adai Huwa Anakojoa Kwenye Swimming Pool


Video queen matata Bongo ambaye ni mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, David Genzi, Tunda Sabasita hivi karibuni alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram, akitamka maneno ambayo watu walimshangaa na kudai kuwa anatia aibu.

Mrembo huyo ambaye alitupia video hiyo akiwa kwenye jakuzi na Mtangazaji wa Radio Choice FM, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ wakati akiogelea, alitoa kichwa kwenye maji na kuanza kuelezea kuwa hakuna kitu kilichomkera kama jakuzi hilo kuwa na maji meupe badala ya bluu ambayo huwa akitoa haja ndogo haionekani.

Baada ya kupewa za uso na watu walioiona video hiyo, Wikienda lilimwendea hewani Tunda ambapo alisisitiza kuwa alichoongea ni kweli kabisa na hata siyo yeye peke yake bali ni watu wengi wanapenda kufanya hivyo kwa hiyo wasimshangae
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Masikini akipata na natako hulia mbwata upo hapo?Nyerere aliwaambiaga watu mkawa mnamuona ni kishoka/mkomunisti sasa mmetaka mambo yaende kama ulaya eh mkojolea humo humo na bado kuna siku mtaanza kunya humo humo kwenye hayo ma-swimming pool wala sintoshangaa

    ReplyDelete
  2. Utamaduni kama siyo wako hata ukiugeza kivipi itaonekana au kujulikana tu kuwa original siyo utamaduni wako hope hayo maji yanayokojolewa yanatiwa dawa mara kwa mara ili watumiaji wasipatwe na magonjwa ya ajabu ajabu duh!Kweli balaa duniani wa jamani

    ReplyDelete
  3. Huyo ni ushamba msione watu kuwa mstaa mukadhani siyo washamba.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad