Vijana, Wadau Kumchangia aliyemtukana Rais Magufuli

Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.

Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.

"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii ni nini?maana yake mnakubali rais wamtusi?mimi si M-TZ but what i can say ni muombe kwa ajili ya Magufuli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanaohamasisa michango ndio walimtuma atukane,ingekuwa tofauti na mawazo yangu kama wangekuwa na utamaduni wa kuchangia vitu vingine kama wenye ulemavu wa ngozi,wajane nk.

      Delete
    2. ni kweli kabisa kila kona ya nchi inachangisha kwaajili ya kuonyesha ya kwamba sheria hiyo siyo sahihi hata kidogo ni sheria kandamizi inayoumiza watanzania na kuwanyima uhuru wa kuongea.... yaani unapangiwa cha kusema na ukisema neno linalomkera mtawala haupo salama ila mtawala akikuita kilaza ni sahihi kabisa huna pakumpeleka....

      Delete
    3. ni kweli kabisa kila kona ya nchi inachangisha kwaajili ya kuonyesha ya kwamba sheria hiyo siyo sahihi hata kidogo ni sheria kandamizi inayoumiza watanzania na kuwanyima uhuru wa kuongea.... yaani unapangiwa cha kusema na ukisema neno linalomkera mtawala haupo salama ila mtawala akikuita kilaza ni sahihi kabisa huna pakumpeleka....

      Delete
  2. mmekosa kazi ya kufanya inaelekea mlimtuma kumtukana rais

    ReplyDelete
  3. Tatizo bongo oya oya nyingi sana ,yaani sometime watu wanafanya vitu utafikiri wamekatwa vichwa.Ila naaamin mungu yupo JPM

    ReplyDelete
  4. Ukawa inaonekana upumbavu wao,siasa ni siasa na sisi waTanzania tuna heshima kwa kila mtu,ikiwa ukawa wanataka kuvunja heshima sio kwa raisi wetu jee wao watakubali kuvunjiwa heshima?Wengi sio wana siasa.Mzee Msimbazy

    ReplyDelete
  5. Duh huyo diwani hatari sana sijui anaifundisha nini hata familia yake ni aibu kwa kiongozi kama huyo kusupport ujinga huo looooh ndiomana kizazi hiki kinapiga hata wazazi wao

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ni slave au umetumwa au unajifunza kuropoka kama magufuli?mheshimu anaekuheshimu tumempa kura leo sisi watoto wetu wamekua vilaza?kuna kamusi inasema bwege ni tusi? Au ni sifa ya mtu mwenye

      Delete
    2. PUMBAVU HUNA AKILI HATA WAZAZI WAKO HUWAHESHIMU, MROPOKAJI NI WEWE ULIYE MJINGA WA KUPINDUKIA MSHENZI MKUBWA KAJIFUNZE KUHESHIMU WATU WAZIMA NA VIONGOZI WAKO CHIZI MKUBWA, MAGUFULI SIYO SAIZI YAKO BWEGE WEWE

      Delete
    3. Wewe uliyesema Maghufuli anaropoka utakamatwa wakati wowote labda usiwashe simu au comp yako, na hiyo device labda uitupe, hata ikipita mwaka tutakukamata na sheria itakayo kufunga ni ya matumizi mabaya ya mtandao. Nitakuja kuona wenzako watakavyo kuchangia. Wewe faini yako ni milion 100,000,000 au miaka 25 gerezani au adhabu zote mbili. Nimeamua kukuambia kuwa ukae unajua wewe ni WANTED na Comment zako zimehifadhiwa kama ushaidi wako wa kkuzika ungali mzima. Pole sana ndugu umeyataka mwenyewe mpaka muishe kwa ujinga wenu na mapuuza. Mbona umtukani mzazi wako, kwani kila siku kila kitu anafanya sahihi? angalia kijana unakwenda pabaya tumia vizuri mtandao kwani unajua wenzako wanakamatwaje? acha kucheza na JPM aliwaambia kuwa nyie bado hamjaamka sasa mtaamuka kwa kanuni na sheria tu na ndiyo maana madam r Tulia kakalia kiti nyie mnaishia uwani aibu kwetu tuliwachagua kwenda bungeni kuleta COMEDY, badala ya kujenga hoja za msingi. Kaambukizwa ugonjwa mbaya Mhe, Zitto hadi Kigoma tunamshangaa kutwa anatafutwa na polisi ndicho tulichokuchagulia kutuletea ngoma za kupunga mashetani? waacche hao waendelee na mkakakati wao wa kujiondoa katika siasa na kuwa wana harakati,matokeo yake wanaharakati hawana kazi ya kufanya, jamani watakufa na njaa.

      Delete
  6. Upinzani ndo wanondoka kwenye Ramani. Wanapotea muda si mrefu, trend yao toka wamemaliza uchaguzi haijakaa sawa. R.I.P Upinzani. You are totally eroded

    ReplyDelete
  7. Mie naomba kujua,, KILAZA ni Tusi au sio tusi,? BWEGE ni tusi au sio tusi? LOFA ni tusi au sio tusi? MPUMBAVU ni tusi au????

    ReplyDelete
  8. Mie naomba kujua,, KILAZA ni Tusi au sio tusi,? BWEGE ni tusi au sio tusi? LOFA ni tusi au sio tusi? MPUMBAVU ni tusi au????

    ReplyDelete
  9. Upinzani mnachemka vibaya,bado kidogo mtakauka kama sio kuungua.
    Hatuwaoni mkijitokeza kwenye kuchangia jamii mahitaji ila kwenye hii ya kumtukana Rais ndio sawa?Hapana jamani,mmechemka!

    ReplyDelete
  10. Hayo maneno kamwambie mzazi wako au ndugu yako hapo utajua maana ya maneno hayo. Hap hakuna mwalimu wote tumeenda shule tunatakiwa kuyajua maneno hayo kabla ya comment zetu. Kaka jaribu kama nilivyo kushauri halfu utatuma matokeo yake kupitia njia hii.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad