Wabunge UKAWA Wasusa Futari ya Waziri Mkuu

Wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa jana walisusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ikiwa ni mwendelezo wa hatua za kususia shughuli zote zinazoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Riziki Ng’wale, alisema wamechukua hatua hiyo kutokana na Dk Tulia kuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo.

“Dk Tulia ndiye mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kufuturisha na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki shughuli yoyote inayoongozwa naye,” alisema muda mfupi baada ya kutoka katika kikao cha wabunge wa kambi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema wamekubaliana wabunge wote wa kambi ya upinzani waliofunga watakwenda kufuturu majumbani kwao.

“Tumekubaliana hatutakwenda kufuturu bungeni na kila mbunge atakwenda kufuturu nyumbani kwake,” alisema.

Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha wapinzani kilichoketi chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.

Futari hiyo ilitangazwa na Dk Tulia tangu juzi na kusisitizwa jana baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa mchana kuwa ingefanyika kwenye viwanja vya Bunge ambako wabunge wote walialikwa.

Kwa siku zaidi ya 10 sasa, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk Tulia kwa sababu hawana  imani naye.

Hali hiyo imefanya bajeti kuu kwa ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuchangiwa na wabunge wa CCM tu baada ya Dk Tulia kuongoza vikao kila siku, akiingia asubuhi na jioni.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hamna akili nyie wabunge wa upinzani futari na Tulia wapi na wapi au mnayenu mseme

    ReplyDelete
  2. akili za hawa jamaa wa ukawa sijui wamezitoa wapi yaani hawa sio kabisa

    ReplyDelete
  3. suseni tu kwani nani anawahitaji

    ReplyDelete
  4. wanabuluzwa na Mbowe hao

    ReplyDelete
  5. na wamebuluzika kweli

    ReplyDelete
  6. Siasa imeingiaje hapo kwenye futari jamani?

    ReplyDelete
  7. ninachowashangaa wabunge wa ukawa ni kwamba mnashindwaje kuevaluate strategies zenu na kuona kama zinazaa matunda au lah! sababu tangu mlipoanza kutumia mbinu ya kususia bunge mpaka sasa ni muda umepita na haijawahi zaa matunda kwenu wala kwa wananchi mnaowawakilisha hivo kwa nini msikae chini na kutafuta mbinu mbadala ya kutoa malalamiko yenu badala ya kususa? Mmechaguliwa na wananchi ili mkasusie vikao.

    ReplyDelete
  8. Ahhhhhh.. Nimesikitishwa na hiki kitendo... Tena sijakitegemea Kwetu hapa TANZANIA.

    Kwa sisi Watanzania na jinsi tulivyo lelewa na kulea watoto zetu. Tofauti ya Dini haina gap kubwa baina yetu .. tumecheza pamoja/ tumesoma pamoja/ tumekwenda jeshini pamoja/ tumefanya kazi za ujenzi wa taifa pamoja.. tumeweza kungojeana kwa baada ya ibada zetu ndiyo tuanze safari yetu kama ni za matembezi au kutembelea wagonjwa mahospitali.. Na hii tumedumunazo katika maisha yetu na tumeweza kuheshimu dini na ibada zetu ipasavyo.

    Mwezimtukufu wa Ramadhani ni Moja ya nguzo ya dini yetu ya Kiisalamu ambayo tunafundishwa toka utotoni na inatujenga kuwa wavumilivu na wastahamilivu na kuweza kujiweka na kumjua aliye na halii duni zaidi maisha upande wake yakoje..Na mwezi wa ukarimu na karam... mwezi wa kusameheana na kuoba maghfrira kwa mola wetu na kuzidisha ibada na kuweza kuwa karibu na familia na Jamii na watu wako wa mji wako na mikoa yanu na Taifa lenu na ulimwengu kwa ujumla..Leo nikikwambieni hapa Obama anaalika wana Diplomasia wote Wa nchi za Kiislamu na wasiokuwa hii ni kwaajili ya Nini? inathibitisha kuwa Tunaheshimu na kuelewa Ramadhani ni Nini halafu pia inaashiria kuwa Dini zetu hazitutenganishi sisi wote ni wamoja na isitoshe inajenga Imani katika maelewano baina ya watu.. Hivi siku chache zilizo pita nilikuwa Malaysia.. Nilipendezewa sana baada ya sisi kualikwa baadhi ya walioalikwa walikuwa ni waMalay wenye asili za Kichina na Kitamil na waarabu niliuliza jee hawa wote wanafunga? Jibu lilikuwa Zuri sana na nikafurahi.. Sisi hapa Malay/Mchina? Muhindi/ Mwarabu / wote ni wamoja na kila mwanajamii wetu katika wakati kama huu anamsapport mwenzake bila kuonesha kasoro..Akaanza kunieleza Historia ya nchi yao baada ya kushikwa na Dr Mahathir Mohammed to katika ukulima wa Rubber tree /Minazi na Mawese mpaka leo Malaysia ni Moja ya Economical Giants of South East Asia.. Nilimuuliza vipi iliwezekana na kwa muda gani... Na kilicho endelea nilisikiliza na huku siamini naamini .. Ilichukua miaka karibu @0 na kidogo.. yote ilikuwa ni kwamba watu walibadilisha Working Culture wakawa wote wameondoa Tofauti zao za vyama .. na aliitwa Dikteta kwa ajili wa wavivu wasiotaka maendeleo na wapenda kusema na alikandamiza panapo hitaji kukandamiza ili alete maendeleo ya jamii na watua baada ya kuona mambo yanakwenda viwanda vinafanya kazi ajira inapatikana .. WAkaondoa tofauti zao na kuanza kujituma zaidi na kina mama wakaaza kukatiwa barabara za toll kwa kilometa na ajira ikawa kila mwanafamilia anawajibika nchi ikawa haina tena gumzo ni kila mtu kazi kwa shifts kila nyanja.. mkulima wa Rubber tree ameondolewa tax na anafatwa huko huko shamba kwa huduma zote shule/hosp/benki/huduma zote sa rekikali na wana serikali yao ya kitongoji kuwathibiti vijana viongozi wa kesho kama iliyofanywa hapo Siha (Kilimanjaro) na Kasalazi (Sengerema) ili kuwaweka katika Maadili hata watakapo fikia wakati wa kuwa watendaji ni kwamba wameshapata Malezi bora na imani bora ya dini zao bila tofauti na ni Taifa Moja na Mwelekeo Mmoja... Na Mpaka sasa Haya ndiyo Maisha yanayo endelea... Hili wa Watanzania Kususiana Futari na Kudhalilisha IMANI kwa kuonesha Kuto Heshimu Mwaliko wa kuadhimisha Moja ya Nguzo ya Dini Yetu ya Kiislamu Hapo Nasema HILI SIYO SAWA NA HALIKUTEGEMEWA KUINGIZWA KISIASA NA SIYO SIASA .. Bila kumtaja jina mmoja wa Waziri wa Awamu ya Nne ambaye tulikuwa Marafiki to kato utotoni... Alikuwa Dini Nyingine na Mimi ni Muislam.. Ilikuwa yeye ananikumbusha wakati wa Sala na tunatoka pamoja kwenda msikitini na ananingoja mpaka namaliza kusali nalafu tunaendelea na mengine hii imejenga Undugu baina yetu na watoto zetu na familia zetu. Na Tofauti baina yetu hakuna ni tumekuwa ndugu hata Vijana wake wamekuja kusoma Na tumeishi nao bila kuona tofauti kuwa mie si mzazi wake.. Anaona ni mzazi na akimaliza anarudi kujenga Taifa.. Naomba toufauti zetu Tusizilete katika HAYA... TANZANIA NI UPENDO / AMANI/ UMAOJA NA USHIRIKIANO WA MILELE.

    ReplyDelete
  9. Daaaahhhh... Yaani Mmemchukia Tulia Kiasi kwamba Hamkwenda kwa Majaliwa Kiasa tulia yuko!! Kama ni hivyo itabidi mwandike barua za kujiudhuru na kutajulisha waliowaleta hapo(wapigakura wenu) kuwa samahani ninajiuzulu kwa ajili nimeshindwa kutoa ushirikiano wangu na Dr Tulia... Hatuwivu chungu kimoja kwa hiyo nitaomba kura zenu huko2025 kama bado sijachoka.. tena hizo balua mziandike halaka..

    KITENDO HICHI KAMA NI KUBURULZWA NA MBOWE BASI NI KOZA TENA KUBWA NA UPOTOFU WA KUTO SHIRIKIANA KIJAMII NA KIIMANI/....... POLENI KWA MLIOFANYA .. NA SISI HATUKURIDHISHWA...

    ReplyDelete
  10. mtoto wa kike anawahenyesha watu wazima makubwaaaaaaaaa. wana susa susa kama watoto. halafu mnategemea wawasaidie kwenye majimbo yenu haoooooo

    ReplyDelete
  11. Wangeenda kufuturu hapa pangejaa ya kwamba wanapenda kula haaaa haaaa siasa hizi ni balaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad