Wabunge Wataka Clouds Tv Iadhibiuwe Kwa Kufanya Mahojiano na Kijana Ambaye ni SHOGA


WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja.


Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga.


“Napenda kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata muongozo wako,” alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana huyo anajutia kufanya vitendo hivyo.


Alisema mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurahia kitendo kile, na jambo la kusikitisha asubuhi hii (jana), mwendeshaji wa kipindi hicho alialikwa katika kipindi cha asubuhi cha kituo hicho, badala ya kuomba radhi ameishia kujitetea.


Kutokana na maelezo hayo, aliomba Mwongozo wa Spika pamoja na Kanuni na kwa kuwa serikali ipo, itoe kauli kama inaruhusu ushoga au kama hairuhusu ni hatua gani inachukua kwa kituo hicho ili iwe fundisho kwa vingine.


Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Maro (CCM) alisema kijana huyo aliyehojiwa na Kipindi cha Take One cha Clouds Tv amewaaibisha wakazi wa Musoma mkoani Mara, hivyo aliiomba serikali imchukulie hatua kwa sababu anaweza kuwafundisha tabia zisizofaa vijana wengine.


Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akijibu miongozo hiyo, alisema jambo hilo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NI KWELI KABISA INATAKIWA KUPEWA ADHABU KALI!! KUMBE HATA WABUNGE WAMELIONA!!!

    ReplyDelete
  2. NI AJABU MTANGAZAJI BADALA YA KUOMBA MSAMAHA ANAJITETEA!!!

    ReplyDelete
  3. Mmmh kulikoni hao waBunge wanacho hofia nini kama mambo ya mashoga yapo nje nje kwa sasa wala hakuna siri tena mi sioni vibaya wakaliongelea hila hofu wangu ni kwa hao wa Bunge juu sasa mambo yao yatatokea peupe juu wao ndo wana tembea na hao mashoga na kuwapa dau kubwa ndo maana wabunge sasa roho ziko juu juu wakiogopa tutangazwa na hao mashoga yani siri yote itajulikana na kwa vile mashoga hawana siri lol kaeni mkao wa kula.

    ReplyDelete
  4. Mmmh kulikoni hao waBunge wanacho hofia nini kama mambo ya mashoga yapo nje nje kwa sasa wala hakuna siri tena mi sioni vibaya wakaliongelea hila hofu wangu ni kwa hao wa Bunge juu sasa mambo yao yatatokea peupe juu wao ndo wana tembea na hao mashoga na kuwapa dau kubwa ndo maana wabunge sasa roho ziko juu juu wakiogopa tutangazwa na hao mashoga yani siri yote itajulikana na kwa vile mashoga hawana siri lol kaeni mkao wa kula.

    ReplyDelete
  5. Waanze na mashoga walioko bungeni kwanza
    Kwani huko bungeni hakuna mashoga
    Wabunge wengine fyuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  6. Ama kwa hakika ukweli unauma! Huyo shoga anayomengi ya kusema na watu kujifunza, binafsi sikujua kwamba muhimbili kuna NGO inawahudumia kwa vilainishi, kondom, mouthwash nk ili waifanye hiyo shughuli yao kwa usalama! Halafu wanaume wengi wanaojifanya kusema maadili yamekiukwa, ndio hao wanao watumia hao mashoga, povu linawatoka kuhofia pengine atawataja majina. Ushauri wangu kwa Zamaradi, hebu mtafute tena huyo shoga atutajie majina ya mabwana zake, kama hatutabaki midomo wazi.....

    ReplyDelete
  7. Mashoga wapo na sioni cha ajabu kwanini mashoga wasiojiwe kama watu wengine. Wala sioni sababu ya bunge kujadili jambo kama hili wakati wana mambo makubwa na ya muhimu zaidi....

    ReplyDelete
  8. DO NOT entertain them, wapo sara basi kunahaja gani ya kuwatangaza hazarani? hii ni ukiukaji wa maadili ya dini na ya kitanzania kwa ujumla, kwani watanzania tunapenda vitu vya kuiga sana kutuka nje, tumasahau kama wao hawana madili.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad