Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.
Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.
Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Sawa kabisa wabunge Mtakoma kuropoka ropoka sasa mtumie akili na kuelewa nini maana ya bunge. Wabunge vilaza Mtakoma awamu hii. Hapa kazi tu
ReplyDeleteKoma wewe kuna wabunge wambeya na waropokaji , udaku, mipasho, Kama ccm
DeleteFyuuu
Simamisha sana lakini huwezi kuwafukyza ubunge tumewachaguwa
ReplyDeleteHawakuteuliwa
Kaaaaaa vikao vyote vya bunge mpka 2020 hutuoni ngoooooooii
Kama posho kanzie mtaji wa kugombea ubunge jimboni
Nidhamu Nidhamu Elimu Elimu Elimu .Jiheshimu Jiheshimu Uheshimike Muheshimiwa na kuwa Mzalendo wakati wote na matendo yako yote yaelekee huko kwenye uzalendo.
ReplyDeleteBunge limeshikwa Na raisi halina mamlaka kabisa Kama zamani
ReplyDeletekilaza mkubwa wewe, rais anahusikaje kwa hilo???????????? mfyuuuu
DeletePunguani nani aliyempa bu ge raisi
DeleteThis new era of leadership... Upuuzi na Upumbavu hatuuvumilii kutoka kwa watu waliopewa dhamana na wananchi (MP).. Tunataka wawe wakweli na wajue wanasema nini na kwa faida ya nani... Ukweli ni kwamba mwelekeo wote uwe ni wa kuleta Maendeleo na si vinginevyo mpo Waheshimiwa!!! NA KA HUWEZI UNAACHIA KAMBA MWENYEWE.
ReplyDelete