Wabunge Wengine Wawili Wasimamishwa Kuhudhuria Vikao

Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.

Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.

Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa kabisa wabunge Mtakoma kuropoka ropoka sasa mtumie akili na kuelewa nini maana ya bunge. Wabunge vilaza Mtakoma awamu hii. Hapa kazi tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Koma wewe kuna wabunge wambeya na waropokaji , udaku, mipasho, Kama ccm
      Fyuuu

      Delete
  2. Simamisha sana lakini huwezi kuwafukyza ubunge tumewachaguwa
    Hawakuteuliwa
    Kaaaaaa vikao vyote vya bunge mpka 2020 hutuoni ngoooooooii
    Kama posho kanzie mtaji wa kugombea ubunge jimboni

    ReplyDelete
  3. Nidhamu Nidhamu Elimu Elimu Elimu .Jiheshimu Jiheshimu Uheshimike Muheshimiwa na kuwa Mzalendo wakati wote na matendo yako yote yaelekee huko kwenye uzalendo.

    ReplyDelete
  4. Bunge limeshikwa Na raisi halina mamlaka kabisa Kama zamani

    ReplyDelete
    Replies
    1. kilaza mkubwa wewe, rais anahusikaje kwa hilo???????????? mfyuuuu

      Delete
    2. Punguani nani aliyempa bu ge raisi

      Delete
  5. This new era of leadership... Upuuzi na Upumbavu hatuuvumilii kutoka kwa watu waliopewa dhamana na wananchi (MP).. Tunataka wawe wakweli na wajue wanasema nini na kwa faida ya nani... Ukweli ni kwamba mwelekeo wote uwe ni wa kuleta Maendeleo na si vinginevyo mpo Waheshimiwa!!! NA KA HUWEZI UNAACHIA KAMBA MWENYEWE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad