Wapinzani Wawasilisha Hoja ya Kumwondoa Madarakani Naibu Spika, Dr Tulia Ackson


Wabunge wa upinzani wamewasilisha kwa Spika wa Bunge hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye.


Hatua hiyo imefikiwa na wabunge hao kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa uongozi wa Dk Tulia anapokalia kiti cha Spika.


Tangu Jumanne wiki hii, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo kwa madai anaminya demokrasia.


Walifikia uamuzi huo baada ya Dk Tulia kuzuia kujadiliwa hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi zaidi ya 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) iliyowasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na kukatisha mjadala wa bajeti ya maji.


Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wote wa upinzani kupingana na maamuzi ya Dk Tulia, jambo lililosababisha watolewe bungeni.


Kutokana na hali hiyo wabunge hao kupitia Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya akisindikizwa na Mbunge wa Kibamba, John Myika wa Chadema na Mbunge wa Konde wa CUF, Khatibu Said Haji waliwasilisha hoja hiyo kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah baada ya Spika, Job Ndugai kutokuwapo bungeni.


Hoja hiyo iliwasilishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 138 (1) ambayo inaeleza utaratibu wa jinsi ya kumwondoa Naibu Spika.


Kanuni hiyo inasema, “Utaratibu wa kumwondoa Naibu Spika madarakani chini ya Ibara ya 85(4)(c) ya Katiba utakuwa kama ule wa kumwondoa Spika, isipokuwa tu taarifa ya kusudio la kumwondoa Naibu Spika madarakani inayoeleza sababu kamili za kuleta hoja hiyo, itapelekwa kwa Spika ambaye ataiwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuijadili.”


Fasili ya pili ya Kanuni hiyo inasema:“Endapo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Naibu Spika zinazohusu uvunjaji wa Katiba, Sheria au Kanuni zinazoongoza Shughuli za Bunge, basi Kamati hiyo itaidhinisha kuwa hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.”


Kwa mujibu wa Ibara ya 85(4)(c), Naibu Spika atakoma kuwa Naibu Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika endapo ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu Spika kwa azimio la Bunge.


Akizungumzia uwasilishwaji wa hoja hiyo, Millya alisema taarifa zaidi watatoa leo kuhusu msimamo wao huo.


Dk Tulia aliwataka wabunge wenye malalamiko juu ya utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za Bunge kukata rufaa kwa kufuata Kanuni za Bunge.


Alisema kanuni ndogo ya 5(2) inasema Spika atawajibika kutilia nguvu kanuni zote za Bunge na 5(3) inasema Spika anaweza kumtaka mbunge yeyote anayekiuka kanuni hizi kujirekebisha mara moja.


Alisema kwa hiyo mbunge yoyote asiyeridhika, kanuni za Bunge zinamruhusu kukata rufaa na zinamweleza nini cha kufanya.


Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tulia hawezi kuondoka kienyeji hivyo wapinzani kama mnabisha mtaona mnapoteza muda we4nu bureeeeeeee kalaleni kama bunge hamliwezi tatizo vitoto vingi upinzan, mamburura tu nyie

    ReplyDelete
  2. Hii mkiipuuza mnaua Taifa la kesho.inabidi watu waandamani.hawa ni watoto wenu wanaopotezewa muda ma pesa. Si mtu mmoja mwenye amri kukatisha maisha ya watu 7,000.na wabunge wote wa ccm hamlioni kosa.inatia aibu na mmekuwa tatizo la serikali.mnaweza kuwa CCM lakini hakuna mwenye fikra huru. Ni utumwa udiosemeka na ujinga wa konamna yake. Hii ndiyo jamii mnayoiwakirisha bungeni.hamoni ni kosa kubwa.uongozi ni nini mula milala.hamfai kuwa bungeni kama mnashindwa kuwatetea waliowapeleka. Ungeni. Ni kujasa pesa bila kuzifanyyia kazi. Ni wizi wa kinamna yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wanatafuta kiki nilichofurahi hata wakisusa vikao vinaendelea patamu hapo.umesikia rais alivyosema wewe bwege unayetetea akina mboye,kasema mtafiti kutoka chama cha ACT wazalando alisema hiyo program ibebe wanafunzi 1500 tu wao wakazidisha watoto 7500 kwahiyo walimu wamelemewa,upande waselikali wamewawajibisha watendaji wazembe sema tu kuwapa watoto masaa 24 nami napinga.kingine rais anasema amefanya uchunguzi waliopelekwa kusomea hiyo kozi ni vitoto wa vigogo wasio kuwa na sifa wenye sifa ni watoto wa maskini wameachwa.sasa ninachokiona kwa wapinzani wanakwenda kwa matukio hawafanyi research wanakurupuka tu ,mwenzao kafanya research.sasa wanafanya uchunguzi wenye sifa watarudi wasio na sifa waende vyuo vya stail zao ndipo utaona ni jinsi gani watoto wa vigogo wanatimuliwa.magufuri nampenda sana .mimi nipo upinzani ila kwa hii hali inakoendelea tunapoteza mwelekeo.

      Delete
    2. Kukatisha maisha ya watu 7000 kivipi weweeee Anonymous 12:51 PM. Hawa wanafunzi 7000 wote ni vilaza. Hawana credintials enough za hadhi ya kuwaweka hapo Chuo Kikuu. Wamewekwa hapo kwa vigezo tu vya wazazi wao ambao no wadosii.Wale watoto wa maskini ambao wanazo credintials za kuwaweka hapo hawapo. Sasa unategemea nini. Watoke huko wakahakikiwe upya ili tujue pumba ni zipi na mchele ni upi. Huwezi kwenda kutoa mamillion ya pesa za mikopo kwa vilaza. Ni kitu ambacho hakiingiii akilini hata kidogo. Sasa unataka watetewe, Watetewe na nani labda vilaza wenzao. Haina haja ya povu kukutoka. Majina yatahakikiwa na wale wenye sifa zinazostahili watarudishwa pale Chuoni.

      Delete
    3. Wewe Anonymous 12:51 PM Mchezo huu hauhitaji hasira. Nyamafu mkubwa weeeeeeeeeeeeeee

      Delete
  3. Tatizo hapo sio Naibu Spika Dk. Tulia Ackson. Tatizo ni kasi ya Rais.Magufuli. Ile hoja ya HAPA KAZI TU inawapa shida sana. Na wataisoma namba mwaka huu.

    ReplyDelete
  4. waondoke wao tumewachokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  5. Dkt. Tulia ni mama Jasiri mtendaji wa kazi anaye jali maslahi ya taifa kwa kungalia mada na maudhi..baadhi ya wachache kama si mmoja au wawili wameona kasi yake na utendaji wake unapinga mchezo mchezo walio zoea miaka ile..Sasa napenda watambue kuwa hii Tanzania ya awamu ya tano..inarudisha nidhamu na uwajibikaji na unaweka standars as par..msioweza mtamuona mama kuwa Noma..na kama hamuwezi tafadhalini msitulie posho na upoteshaji...mama Tulia yuko Tuli na Makini...MSITUCHEZEE NA KUTUIBIA WAKATI..MPO

    ReplyDelete
  6. DKT Tulia kwanza ukiangalia mtu mwenyewe ni msomi dr na hana mchezo wao walitegemea kuendelea na zama za serikali ya awamu ya nne kumbe sio hii ni serikali ya awamu ya tano lazima muelewe halafu niwaulize MBOE, LISU MDEE, LEMA, MNYIKA ebu wekeni CV zenu za elimu tuone elimu zenu zilivyo ndio tuwape ushaur pengine tunawaonea maana ninacho jua tuli ni dokta sasa wenzangu na nyie nin akina nani au tuwaite viongozi wa kambi rasmi bungeni labda ndio ngazi ya elimu ninayoweza kuwapa hamumuwezi dr

    ReplyDelete
  7. hiyo hoja pelekeni kwenye familia zenu labda huko mnaweza kupata sapoti

    ReplyDelete
  8. kasi inawatesa sana wapinzani

    ReplyDelete
  9. mlichukulia poa serikali ya awamu ya tano eeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  10. Waheshimiwa hebu mkae na kutafakari maamuzi yenu.Nionavyo mie mnatupotezea haki yetu sisi wanawanchi, kumbe ziko taratibu na kanuni kweli mnazichambua na kuzielewa au action kwanza halafu kutafakari matokeo baadae!! Tumewapa kero zetu mkazipeleka Bungeni, sasa hata majibu kutoka kwa Mawaziri mnayakimbia......Wakati mwengine huyo Kiongozi wa Kambi ya Wapinzani anapotoa pendekezo/wazo lake kwenu siyo lazima mlichukue zima zima kama linavyokuja mbona wengi wenu mmemaliza madarasa yote jamani? tunahitaji upinzani makini Bungeni kwa mustakabali wa demokrasia na maendeleo yetu waTz. WE NEED U THERE ON FULLTIME BASIS Waheshimiwa na muache dharura dharura.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad