Watumishi 12,246 Waondolewa Kwenye Mfumo wa Malipo ya Mishahara Serikalini

WATUMISHI 12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa sababu mbalimbali, ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kumalizika kwa mikataba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angela Kairuki alisema kuondolewa kwa watumishi hao kumeokoa Sh bilioni 25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao.

Alisema kuwa fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo, ikilinganishwa na watumishi 10, 295 walioondolewa kwenye mfumo kuanzia Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu.

“Jumla ya Sh bilioni 23.2 ziliokolewa kwa kipindi cha Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu baada ya Rais John Magufuli kutoa maagizo ya kuwaondoa watumishi hao kwenye malipo,” alisema Kairuki. Alisema pia kuwa watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni pamoja na Sh bilioni 1.8.

Alifafanua kuwa ofisi hiyo ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwasilisha taarifa ya watumishi hewa ifikapo juzi (Juni 10 mwaka huu).

Alisema kuwa walielekeza taarifa zibainishe majina, namba za hundi za watumishi hewa, tarehe walizotakiwa kuondolewa kwenye mfumo, kiasi cha fedha kilichopotea na kilichookolewa.

Akizungumzia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Waziri huyo alisema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa na dhana ya mchango wa watumishi wa umma katika uchumi.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa mama! Huu ndio mwelekeo tunao utaka. Uko. Vizuri kabisa katika uwajibikaji.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Angela mama
      Kina margret Sitta wataitwa Nani

      Amshukuru Riziwani
      Fyuu
      Zanaki ina mambo

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad