Waziri Mkuu: Tutakuwa Tunatumia Kiswahili Kwenye Mikutano ya Kimataifa, Tutaajiri wa Kututafsiria

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaanda mikakati ya kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa. Ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Zainabu Vulu Bungeni mjini Dodoma.

Amesema Kiswahili imekuwa sasa na ni lugha ya sita au ya nane kwa matumizi duniani, na watakuwa wanaenda na watafsiri wakienda safari za nje na kuwapa vijana ajira. Video:

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata haitaji kusafiri na watu tupo tele watanzania ughaibuni tumesoma na tuzijua lugha nyingine zaidi ya kiiengerza
    Balozi zetu zitangaze nafasi hizo
    Ila chonde chonde wakenya wasipewe kwani ni hodari wa kudandia Dili na Kiswahili chao si bora Kama chetu

    ReplyDelete
  2. MH.Majaliwa nalikubali Sana..nikweli ligha yetu Ni lazima tujivunie hayo Na tuipeleke Duniani..Na sisi Watanzania ndiyo chimbuko Na tunaielewa vilivyo..Fikra Ni nzuri Na tutaanzusha taasisi za kufundisha lugha yetu kwa wageni Na itasaidia maendeleo Na kujenga ajira..Asante kwa Hili Ni Safi Sana..

    ReplyDelete
  3. Wazo zuri,lakini tunaomba wazungumzaji wajue kutumia herufi "l" na "r" au sivyo mtafsiri atakuwa anatafsiri visivyo. Mfano, mzungumzaji asiseme "kula" wakati anatakiwa aseme "kura"(kwa kiingereza: eat/vote)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na asiseme akuna wakati anatakiwa aseme hakuna, asiseme abari wakati anatakiwa kusema habari, maana naona hii lugha sasa inakufa kila ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utakutana na maandishi ya hivyo!

      Delete
    2. Na asiseme akuna wakati anatakiwa aseme hakuna, asiseme abari wakati anatakiwa kusema habari, maana naona hii lugha sasa inakufa kila ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utakutana na maandishi ya hivyo!

      Delete
    3. Kama tuna viongozi wasiojua kiingereza, haina neno kutumia mkalimani, lakini kama wapo wanaojiweza, sioni umuhimu wa kutumia mkalimani. Kiswahili lugha nzuri, na tunaipenda, lakini inapokuja kwenye maswala ya kimataifa, lazima twende nao sambamba.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad